Unajua kiukweli na kibinadam hebu angalien ingekuwa hayo kayafanya mwanamke ingekuwaje jaman?
N huo udhaifu wa miaka saba ni wa aina gani huo?
Je angekufa huko ingekuwaje?au angenikuta mataizo aliyonisababishia yameniua je angerudi wapi?
Achen bwana,ninawacwac km ulishawahi kupenda tena kwa moyo wako wote alafu ukaumizwa na ukaujua uchungu wake wakati hapo hakuna ndoa,watoto wala mimba!
Alafu hapo mlishapitia magumu mengi labda ndio mmefanikiwa alafu ndio akakimbia!
Kwahilo kwangu ni ngumu sana na hapo tutadanganyana tu hata tukirudiana kamwe sitaweza kumpenda tena,
Labda tuishi kinafiki na binafsi huwa siwezi maisha ya maigizo ni bora niishi kwa shida peke yangu na si kuigiza!
Dina, ulipata wasaa upi wa kumsamehe wakati hakuwepo?? maisha bila yeye hayakuwa rahisi kama mtoa mada alivyoeleza, mke alipitia machungu mengi! kuendelea na utaratibu wako wa maisha kana kwamba yeye bado hayupo ni kwamba bado hujasamehe hapo!
hapa kinachokuja kuumiza zaidi ni majeraha ya tatizo ndo yatakayohukumu zaidi
Bora umelielewa hilo,hapa kinachokuja kuumiza zaidi ni majeraha ya tatizo ndo yatakayohukumu zaidi
swali langu ni je pata picha mama yoyoo kakukimbia miaka 7 na amereje anataka umsamehe mrudiane! Utamsamehe? Vp utaishi nae? (uzungumze ya moyoni mwako) na hapo alikukimbia ulipokuwa umefulia but now alaa mambo super..nipe jawabu
Sasa kwa mwanaume wa aina hiyo c ndio wrong selection yenyewe!kutendwa sio sababu ya kutopenda tena, kwanini umulike ulipoangukia na usimulike ulipojikwaa?? bado tunarudi pale pale, hatuchagui wenzi wetu kutokana na upendo wa kweli but merely from other minor factors, uzuri, kazi nzuri, fedha, etc ... sasa hapo wakati wa misukosuko ya ndoa kwanini msiangukie pua?? hakuna miujiza hapo ... its purely a wrong selection from the scratch!
Bora umelielewa hilo,
Tatizo ni yeye kutaka kusamehewa,labda angefuta vile nilivyomwambia aondoke na akaondoka,
Akanipa muda mpaka pale nitakapoona au ikitokea moyo wangu ukarudi labda sijui yani hata sijui itokee nn jaman,
Itafutwe namna ya kuweza japo tuwe tunaonea tu na kuwasiliana taratibu na akaweza kunishawishi kuponesha majeraha labda inaweza tokea tukaweza kujadili swala la kuwa pamoja tena,ila nahis inahitaji mda tena labda miaka 7!
Madabwada, kwani kutoa msamaha lazima nitamke mbele yake kuwa sasa nimekusamehe unaweza kwenda? Na ndio maisha hayakuwa rahisi ndio maana najiuliza kuwa yeye ataleta urahisi gani sasa kama sio kuniongezea wingu jeusi moyoni? Angekuwepo wakati tunahangaika na mboga zetu ningesema that's my men, kwa shida na raha. Siamini kama nitakuwa nalipa kisasi kama Husniyo alivyosema kwenye mchango wake coz sioni kama kumkatalia kurudi naweza kufananisha na kuondoka kwake. Na je una maana ila msamaha utimie ni kwa kumkubalia arudi kwenye maisha yetu? Kama ndivyo, basi aende bila msamaha.
hapa kinachokuja kuumiza zaidi ni majeraha ya tatizo ndo yatakayohukumu zaidi
Sasa kwa mwanaume wa aina hiyo c ndio wrong selection yenyewe!
Kwa upande wangu kwa ujaji huo sitaweza kuwa naye,labda aondoke zake mpaka hapo itakapotokea moyo wangu ukafikiri vinginevyo jambo ambalo litakuwa gumu coz bado nitakuwa na majeraha.
Sasa kwa mwanaume wa aina hiyo c ndio wrong selection yenyewe!
Kwa upande wangu kwa ujaji huo sitaweza kuwa naye,labda aondoke zake mpaka hapo itakapotokea moyo wangu ukafikiri vinginevyo jambo ambalo litakuwa gumu coz bado nitakuwa na majeraha.
BPM, healing is gradual process, ni kama kuuguza kidonda chochote kile mwili, maumivu hupungua kadri muda unavyokwenda, hatimaye hupona. Utabakia na kovu, lakini maumivu hayatokuwapo tena!!
unaweza kuuguza kidonda lakini kila ukikiangalia na jinsi ulivyokipata unawez akuumiza zaidi
hahahhaaaaa ... ni kweli, lakini with time utasahau tu. Furaha ni siku utakapo pona kabisa!
kabla ya kutengana ni lazima kuna suala ambalo limepelekea kufikia hatua hiyo na inategemea nani mkosaji maana unaweza ukakosa wewe lakini hatua akachukua mwenzako ... kwa maana hiyo narudi kule kule kidonda / jeraha la wakati wa kuachana ndilo litakalokuongoza kwani hata kama ingekuwa miaka 10 bado kuna mambo wewe binafsi unaweza kuyaangalia na umuhimu na ulazima wa mtu huyo kuwa nae ..
lakini kumbuka nawe unakuwa si malaika hivyo utajikuta umeanzisha mahusiano na hilo nalo litachangia katika maamuzi yako
Lakini ujue si wanaume tunapenda hawa wenzetu watusamehe lakini sie huwa wagumu kweli na matusi juu
ANGALIZO: ukimtelekeza mwanamke mwenye kipato chake ukirudi umeisha jela nje nje umkute kwenye silent mode labda
C heri pia umeelewa maana kama ulikuwa na jeraha kubwa la kuachana unaweza kujikuta unachukua shoka na unamaliza ghadabu zako zote
Hiyo kitu ni ngumu sn,tena ashukuru amemkuta angekuta kaolewa je angemwombaje huo msamaha!alafu wanaume mnateteana ingekuwa ni kinyume chake dah cjui huu uzi ungekuwa page ya ngapi!mie hapo ni kumfukuza tu akaendelee na maisha yake tu ujio wake utanitonesha maumivu upya!
Baba X aliondoka nyumbani kwake miaka 7 iliyopita na kuambatana na nyumba ndogo yake,na kumwacha mkewe akiwa mjamzito miezi tisa na watoto wakubwa wawili, ,bila hata huruma,na hakuwa na mawasiliano yoyote kujua wife na wanawe wanaendeleaje,
,mama wa watu alijifungua mtoto wake salama maisha yakiwa magumu na kuwalea wanae kwa taabu akifanya biashara ya kuuza mboga mboga , mungu si athumani kasomesha mwanae mkubwa sasa yuko form five ,mwingine form two,Na yule alokuwa tumboni sasa yuko la kwanza ,
Juzi mama wa watu akiwa anaandaa chakula mara mmewe huyo after seven years aliyowatelekeza..
Mama kwanza alidhani kaona mzuka na kuanguka chini huku fahamu zikimpotea ,,
Baada ya kuzinduka anakuta jamaa analia huku anaomba kusamehewa.....
eti shetani ndo alimpotosha ,anatubu dhambi zake na sasa anaomba wasameheane waanze upya..:hatari:
Kama wewe ndo mwanamama ulokumbwa na dhahama hili ungefanya maamuzi gani???:A S-coffee: