Wasanii wengi wa bongo wanazidiwa Akili na Diamond sana tena sana,,huyu dogo akili kubwa sana yani kama angefanikiwa kuendelea kusoma naamini angekuwa na PHD kama sio docta kabisa, sababu najaribu kufikiri baadhi ya kazi zake za mziki ufundi anaoutumia kuandika nyimbo zake na hata ile kujua tu huu wimbo utakmata mtaa.. Niliwahi kumsikia ney wa mitego pamoja na utata wake ule alisema siku ambayo amefanya kazi na diamond alikiri wazi kwamba dogo anajua sana mziki
Halafu ukija kuzungumzia alivo kuwa na vision ya mziki aliwahi kusema pia anataka tufike na sisi tufanye show za Dollar elf 30 kama kina psquare,hapo ni wakati huo anaanza kutoka kimziki leo tunaongelea show ya mill100.
Na ukiangalia kwa namna Diamond alivokuwa kipindi hicho anaanza kutoka utaona wazi kwamba macho yake yalikuwa kwa Psquare namna wanavovaa na dansi zao zile kwenye Show kwa hiyo kuiga kwenye mziki ni njia ya mafanikio naye leo amefanikiwa pamoja na kuiga huko.
Haya tukaja kwenye kutengeneza timu ,wasanii wengi hata marekani wana team kubwa ya watu kuanzia manager, organizer, stylist, photographer,make up artist, video director na wengine wengi tu,hapa bongo kuna siku niliwahi msikia msanii akisema manager wa nini na kwanini niwe na team kubwa gharama tu. Lakin Diamond kaweza kuwa na team(hapa ndio namuona dogo kichwa kwa uthubutu)na amefanikiwa.
Pia tukubali tukatae dogo kabadili mziki wa bongo kwa kiasi kikubwa sana wengi walikuwa hawajitambui enzi hiyo hawajui thamani yao malipo ya shows zao sasa yako vizuri..lakini nijitihada zote za dogo.
Mwisho sijaweza kung'amua mpaka sasa kujua ni nani atakuja kuwa the Next Diamond in Bongo maana kijana anavotusua kila leo na hata dalili za kushuka sizioni na wengine hawatokei wa kucompete ,basi tunamuacha tu aendelee kushika chati. Maana hakuna namna.!!