Kwanini tajiri Elon Musk ameweza?

Tangantika

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2018
Posts
5,806
Reaction score
7,429
Elon Musk(Generslist scientist).Mtu pekee aliepuuza dhana ya ubobezi au umaalumu(Specislizaton ) Huyu jamaa amejifunza kila kitu on Earth! Hakuna asichokijua.

Kinachonifurahisha zaidi ni mzaliwa wa Afrika aliehamia marekani kutimiza ndoto zake.AliandaliwA kama mwana sayansi (Physist) lakini kajiongeza uinjinia wa vitu mbalimbali.

Swali la kujiuliza ni vipi aweze kuunda MAROKETİ ya anga za mbali wakati hakusomea hata kidogo wakati sisi waafrika hata walioko Marekani hatuwezi kuunda hata sindano hali tuna mavyuo mengi ya uinjinia barani Afrika.?

Na wengine tunawatuma MİT. Na Oxford kisha wanakuja na wake wa kizungu ndio zawadi wanayotuletea badalaa ya MAROKETİ.

Kumbuka Elon anadhamini tafiti zake kwa pesa yake, usilete visingizio sijui serikali, karibu kwa hoja na povu.
 
Hatujashindwa kuunda, Ila tumeshindwa kujiongeza
 
Elon Musk ni mchapakazi sana na anakwenda kuibadikisha dunia kwa uvumbuzi unaotokea chini ya uongozi wake. Huyu jamaa anamiliki makampuni kibao ya technology. Ni CEO wa Tesla watengenezaji wakubwa wa magari ya umeme, yanayotarajiwa kutawala na kuyaweka magari ya mafuta juu ya nawe. Tesla hutengeneza magari 5000 kwa wiki na huu ni mwanzo tu target ni kutengeneza magari 30000 mpaka 50000 kwa wiki. Elon ana SpaceX ambayo hufanya kama NASA kwenda anga za juu. Boring Company huchimba njia za ardhini za treni na mkampuni mengi tu mengine yeye ni mmiliki. Miaka michache tu Elon atakuwa tajiri mkubwa wa kutisha hata akina Gates hawatamfikia.
 
Juzi tu apa kapunguza wafanyakazi wake almost 3500 kutoka 5000 kwa kuingiza hasara kubwa na kupata faida ndogo.. Kwenye iyo kampuni ya Tesla ya magari.. So sio uhater wala nn ila punguza mihemeko mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwasababu anafuata ushauri wangu
 
Sijaona Kipya! Zaidi Ya Kupambana Kutimiza Malengo Yake Kama Mimi Na Wewe, Hatuwezi Kuwa Sawa ,kila Mmoja Na Safari Yake,
 
Jamaa aje awekeze tz,
Tunajenga s.t. george umeme utakua sawa na bure.
 
Elon ametangaza rasmi hadi kufikia 2025 magari ya mafuta yatakuwa historia ulaya. He he he muradi wa bomba la mafuta soon to be overtaken by "electrifying" events.
 
Elon ametangaza rasmi hadi kufikia 2025 magari ya mafuta yatakuwa historia ulaya. He he he muradi wa bomba la mafuta soon to be overtaken by "electrifying" events.
Hahaha umenichekesha mkuu, umewaza mbali sana, ndio maana Nchi za Kiarabu wanawekeza kwenye vitu vingine saa hizi. Ila Sasa Kuua biashara ya mafuta mpaka wakubwa wa Dunia waamue. Ni mtazamo wangu tu though.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…