Kwako Mheshimiwa Rais.

Ntate Mogolo

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2016
Posts
410
Reaction score
711
Mheshimiwa Rais, napenda kukupongeza kwa ziara yako uliyoifanya mkoani Pwani. Ziara hii, imezidi kudhirisha uchapakazi wako, uzalendo wako na ujasiri wako katika kuliendesha Taifa hili. Pongezi sana Mkuu!

Katika ziara ya Pwani, mheshimiwa Rais, umezindua na kufungua miradi mingi ya maendeleo ambayo ninahakika matunda yake tutayaona. Vijana kwa wazee watakuwa na uhakika wa ajira za kudumu. Pongezi sana!

Mheshimiwa, kuna hili swala la kimaadili uliloliibua kuhusu watoto wakike wanaopata ujauzito wakiwa mashuleni. Mheshimiwa, ninakuunga mkono tena sana!

Mheshimiwa Rais, familia yeyote inayoshika maadili ya dini na mila na desturi haiwezi kukubali ujinga unaoenezwa na propaganda za NGO za kimagharibi ambao utapelekea shule zetu kugeuka kliniki za mama na mtoto. Kwa msimamo wako, watu wote wenye maadili wanakuunga mkono kwa dhati kabisa! Lakini wasio na maadili, watapinga tu kwa vile akili zao zinaamini kila linaloletwa na NGO za magharibi.

Baada ya kusema hao Mheshimiwa Rais! Nimatumaini yangu kuwa, watumishi wote uliowateua kushika nafasi katika ngazi mbali mbali katika serikali yako watalisimamia hili bila kushawishiwa na hizo NGO za kimagharibi! Hawa ni wateule wako, wapo kwenye hizo nafasi kwa kuteuliwa na wewe. Hivyo, hawapaswi kwa namna yeyote ile kupinga hoja, mtazami na kauli yako kwa swala lolote lile, Eti tu, kuwafurahisha watu wa magharibi. Lazima sasa wasimamie maadili yetu kama ulivyoelekeza! Kugeuza shule zetu kuwa kliniki za mama na mtoto, hilo haliwezekani! Wakajaribu kwingine!

Kama watendelea kuonyesha dalili za kukumbatia huo ushawishi wa NGO za magharibi, za kutaka kutuharibia maadili yetu ya Dini, Mila na Desturi zetu basi Mheshimiwa fukuza mara moja! Tunasikia wengine wameanza kuongea kichinichini kama vile kupinga msimamo wako! Timua maramoja! Hatuwezi kucheka na kima, tutavuna mabua!

Mheshimiwa Rais, mimi binafsi nitajisikia fahari sana kama nitakuwa mtu wa kwanza kuteuliwa na wewe kushika wazifa wowote katika serikali yako, kama nitahitajika nikiwa natokea Jamii Forum. Maana ninakuona uko sahihi siku zote katika kulipigania taifa hili!

Washangaze kwa kuniteua! Kila mara huwa ninatamani kuwa kama ningelikuwa kati ya wateuliwa wako, ningechapa kazi kwa bidii na utii mkubwa kwako na ningeyasimamia maelekezo yako yote kwa manufaa ya watanzania wote, kama unavyotukumbusha kila mara, uzalendo na utaifa mbele. Hatuwezi kukumbatia ujinga ujinga unaoletwa na NGO za magharibi. Ninakutakia siku njema.

Mungu Ibariki Tanzania!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…