Habari zenu wana jamvi. Katika pitapita zangu humu jf pamoja na mitandao mingine ya kijamii nimeona vijana wengi tukilalamika kuhusiana na kufanikiwa kimaisha, lakini pia vijana wengi wakiwa wanamshukuru mungu kwa kufanikiwa kimaisha kutokana na mawazo yao tuu.
Swali likaja kichwani kwangu kwanini tunajifananisha na wengine walio fanikiwa, je kunahasara gani za kusimamia uhalisia wako na mawazo yako. Kuna baadhi ya vijana wanaiga watu walio fanikiwa hadi mwonekano, tabia, mavazi na hata hali ya kimaisha.
Lakini kunatatizo gani la kuwa wewe, kunashidagani ya kuyafanya mawazo yako kua chachu ya maendeleo yako tunawaza mawazo mazuri sana ya kiubunifu. Ila kutokana tuu ya kuto jikubali na kumkubali mtuu mwingine unaacha wazo lako na kutaka kufanya la mwenzako ili tuu uwe kama yeye.
Kijana mmoja Mtanzania aitwae isayayunge(wengi wanamfahamu) aliweza kushinda katika shindano la wazo bora la kibunifu linalo tumia mtandao(teknolojia) katika kubadilisha maisha ya waafrika haswa katika suala la elimu na ukimwi.
Kipindihicho raisi wa marekani alikuwa mh george w bush, isaya aliweza kuchukuliwa hadi nchini malekani na kukutana na raisi bush (wakati huo) na kuwasilisha wazo lake la kusaidia afrika.
Isaya aliweza kuwa yeye hakuiga wala kutaka kuwa flani alicho fanya ni kuomba ushauri wa kitaalamu kuliwezesha wazolake liwe tekelezi. Na mwakajana aliweza kupokea zawadi ya heshima kutoka kwa malkia elizabeth katika palace yake nchini uingereza.
Nasasa ni mhasisi na mkurugenzi wa somaapp inayo fanya vizuri duniani kote. Na inatabiliwa atakuja kuwa billioner wa miaka ijayo kwa mujibu wa jarida maarufu duniani la forbes.
Hivyo basi kuwa wewe na ishi mawazo yako. Hatakama maelfu ya watu watakucheka ukianguka simama na simamia wazo lako. Afrika inatuitaji wote na mawazo yetu yakibunifu.by abel kondo
View attachment 984015View attachment isayayunge-20190102-0005.mp4
Sent using
Jamii Forums mobile app