Kuwa makini na Matapeli

Jimjuls

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
486
Reaction score
168
Kuna matapeli wanatumia vibaya jina la kampuni ya World Vision na kudai kwamba wanahitaji uwasaidie kuwanunulia vitu vya kitalii. Huyo tapeli mwenye namba(0788891131) anakupigia simu akidai yupo Serengeti na angehitaji uwanunulie wageni (wazungu) Maasai shuka pc 100 na Vinyago vya Mpingo pc 100. Na anakuambia umsaidie kukutana na Muuzaji amabye yupo Nyegezi nyuma ya Stand ya Mabasi, Mwanza.

Ujumbe wanaokutumia wa awali ni huu hapa chini:

''habari za asubuhi ndugu naimani utakuwa mzima wa afya.nina anko wangu yuko serengeti mbuga ya kitalii ameniomba nimtaftie mtu wa kumsimamia tenda yake nilikuwa namsimamia mimi ila hali yng siyo nzuri kiafya nasumbuliwa na kifua na matezi hata sauti haitoki.ila ni suala la kupata rizki.kama uko tayari niambie nimpe no zako muongee vizuri,'' (Simu namba: 0713804640)

Usidhubutu kufanya nao mawasiliano kabisa.
 
Senzy Kabisa hao! Ilibaki kidogo waniotee.
 
Haya ndio majitu ya kuyapeleka kwenye mashamba ya Magereza yakalime mahindi na mpunga. Matapeli ni watu waovu sana katika jamii. Walimtapeli Mzee mmoja pesa zake za mafao. Mwisho wa siku alifariki kwa msongo wa mawazo. Nawachukia sana MATAPELI.
 
Haya ndio majitu ya kuyapeleka kwenye mashamba ya Magereza yakalime mahindi na mpunga. Matapeli ni watu waovu sana katika jamii. Walimtapeli Mzee mmoja pesa zake za mafao. Mwisho wa siku alifariki kwa msongo wa mawazo. Nawachukia sana MATAPELI.
Duh!Inasikitisha sana.
 
Assist imekua fursa kwa wengi sasa
 
Mkuu ndugu yangu ngoja nitest kumtafuta inaweza ikawa neema kwangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…