hapa sidhani kama utapata info za maana, ongea na wavuvi ziwani uwaskilize wanalaza sh ngapi kwa siku, pia utalazimikak upata wavuvi waaminifu au uwe na ndugu yako anaenda majini, la unaweza kupata wahuni wanauza samaki hukohuko ziwani wanakwambia leo sku mbaya kweli bosi! ongea na wavuvi peleleza.
Humu watu wengi wanajifanya kila Mtu katokea Dar.. Ziwa hawalijui kabisa... huko wanapaita mikoani
Mimi kama nataka kujua kitu very sensitive mfano biashara ya Hiace huwa nauliza Driver au Konda,kama ni biashara ya Kantini huwa nauliza mama ntilie humu majibu si ya kuridhisha hata kidogo utapata ushauri tu zaidi ya hali halisi yenyewe
Mfano kuna mtu alitoa ufafanuzi humu wa kilimo fulani hivi alipotoa makadirio ya Mtaji nikaweka mikono juu ni zaidi ya milioni 20 ya kuanzia Kilimo... mmmmmmmh nilipoenda kwa wakulima kabisa na tena wanatumia mbinu za kisasa hata haikufika milion 8...
Kwahiyo Nenda kwa Wahusika zaidi kuliko humu
Hongera amu,kuwa na uthubutu thabiti,tafuta taarifa sahihi kwa wavuvi na wadau wengine wa mazao ya samaki then utakuwa katika nafasi nzuri ya kuamua. Kemondo si mbali sana,nenda hapo ukate taarifa sahihi.
Kwa laki nne unakodi kwa muda gani ? na je huo ni mtumbwi wa injini au na makasia alafu bado haujatia nyavu .., binafsi mimi sijafanya biashara hii ila najua kununua mtumbwi na injini ni pesa ndefu kidogo na kwa hii mitumbwi ya injini sometimes mtu anakwenda kutupa nyavu anarudi na kurudisha pesa ya mafuta tu (kwahio kupata sio guarantee). Kwa ushauri wangu ili ku-taste the water na kwa mtaji wako kama wateja wapo jaribu kwanza kulangua samaki kutoka kwa wavuvi na kuziuza.., ni mengi yapo huko majini na changamoto nyingi as well as imani za ajabu ajabu
Ushauri wa mdau hapo juu, ni wa muhimu sana, pia ni muhimu kujua hata bei ya samaki au dagaa, inabadika sana, ndani ya masaa huwa inategemea na upatikanaji wa mazao hayo, ukiona biashara inayokimbiwa na muhindi uwe nayo makini sanaHa ha mambo ya kuenda kwa babu kulala uchi?
Anyway mleta data alinipa hilo nkifika ntajua zaidi well mtumbwi hela zipo ila am not risk taker nataka nione inaendaje nimetenga hiko kiasi well ntaendelea.
Nimependa nipe data zaidi
Ha ha mambo ya kuenda kwa babu kulala uchi?
Anyway mleta data alinipa hilo nkifika ntajua zaidi well mtumbwi hela zipo ila am not risk taker nataka nione inaendaje nimetenga hiko kiasi well ntaendelea.
Nimependa nipe data zaidi
Ushauri wa mdau hapo juu, ni wa muhimu sana, pia ni muhimu kujua hata bei ya samaki au dagaa, inabadika sana, ndani ya masaa huwa inategemea na upatikanaji wa mazao hayo, ukiona biashara inayokimbiwa na muhindi uwe nayo makini sana