Kujitibu mwenyewe ni hali ya kuamua kutumia dawa kulingana na ugonjwa au dalili za ugonjwa ambazo mtu anazisikia au anahisi na kuzifahamu yeye mwenyewe pasipo kupata maelekezo ya mtaalam wa Afya.
UKUBWA WA TATIZO
Takwimu za Shirika la afya Duniani (WHO) za mwaka 2015 zimeonesha 80% ya watu (ikiwemo Tz) wanajitibu wenyewe.
SABABU
Gharama za matibabu
Kutumia muda mrefu kupata matibabu kutokana na wingi wa wagonjwa katika kituo cha kutolea huduma za afya
Mgonjwa kutumia dawa zilizobakizwa ama kuachwa na mgonjwa mwingine.
uelewa mdogo juu ya madhara yanayoweza kusababishwa na mgonjwa kujitibu mwenyewe
Vituo vya kutolea huduma za afya kuwa mbali na jamii kwa baadhi ya maeneo
Kutokuwa na Bima na Afya
ATHARI
Mgonjwa kutokupona
Usugu wa dawa aina ya vijiuasumu (antibiotic)
Kusababisha ulemavu na hata kifo
Kuongezeka kwa gharama za matibabu kwa Taifa na jamii kwa ujumla
NI MUHIMU
Usijitibu wala kutumia dawa bila ushauri wa daktari.