Kugombea ubunge kupitia CCM

TOURMALINE

Senior Member
Joined
Jan 4, 2013
Posts
125
Reaction score
24
Mi ni mwanachama wa cCHADEMA nikiwa mjumbe wa chama jimbo mojawapo la mkoa wa Dar.Nina matarajio ya kuomba nafasi kugombea ubunge jimbo la Same Magharibi.

Kwa bahati mbaya wazee wa jimbo hili wameniambia kama nataka kuwa mbunge wao basi niwe mwanachama wa CCM.
Naomba ushauri wenu
Nawasilisha hoja
 
lLumumba FC,tuna mengi ya kujadili si huu upuuzi mnaotuletea
 
kumbuka kuwa watu wengi wanaopiga kura kwenye chaguzi nyingi huwa hawana vyama kwahiyo ni jukumu lako kuwashawishi kwamba unao uwezo kuliko mwingine. kumbuka Slaa walichaguliwa kwy jimbo lake la ubunge wakati CHADEMA wakti huo 1995 kulikuwa na wanachama asilimia 5 na asilimia 80 walikuwa CCM kwahiyo suala ni are you mbunge material au babaisha ----- kama wewe babaisha ----- basi nenda kajiunge na chaka la mafisadi uende bungeni ukubali kutumiwa kama chaka lao la kupitisha maovu dhidi ya nchi hii. lakini mimi ningekuwa wewe ningechagua kuwa kama Obama siangalii namba ya watu weusi iko ngapi bali wote ni wangu na jukumu langu kuwashawishi.
 
Hufai kuwa mbunge.Km umeshindwa figure out hili basi tena.Yaani ukamuulize mchawi,kama mnaweza haramisha nae uchawi.

Km umekuta mzee wa kipare anayeogopa CCM kam sita ni wazi hatokuambia kitu cha kumzidishia hofu.Hawa hawaaminiki kma sita hata nagekuambia bado hupaswi mwamini.

Ungemuonnyes viodole viwili uone anavyokimbia kama anatolewa pepo.Pi ainaelekea hawakujui wakaogopa wakidhni unakwenda mu-Mtwara.Ila ungemuonyesha bendera ya CHADEMA kwanza ,kabla ya kuongea angeweza kushauri.
 
Wamdanganya nani wewe? Wewe ni wale wale CCM. Wapiga kura 2015 vijana watakuwa 60% na wazee watakuwa 12% hao ndiyo wakutishie? Kafie mbali huko.
 
Siamini kwamba kuna wazee wengi wanaoweza kubadili idadi ya wapiga kura. Kwa mtazamo wangu nadhani kuwa ifikapo 2015 idadi ya wapiga kura vijana itakuwa kubwa zaidi kuliko ile ya wazee. hili la kusema kuwa wazee wa Same Magharibi wamekuambia hutapata kura siliamini hata kidogo.
CHADEMA wapo huko na kusema ukweli wananchi wote, wazee kwa vijana wamewachoka mno CCM. Rai yangu kwa makamanda wa CHADEMA ni kuwa waongeze nguvu huko na kuwapa ari ya hali na mali wale wote watakaosimama kwa niaba ya CHADEMA.
 
Mkuu kwani unataka ubunge kwa sababu gani, mpaka usijue chama gani usimamie kati ya CHADEMA na CCM huko jimboni kwako. Hao wazee wamekumbia kwa nini ujiunge CCM? Unataka kusaidia kuleta maendelea huko au unataka ubunge kwa ajiri yako mwenyewe tu kiccm ccm? Chama kipi unakiamini kina sera zilizo sahihi na zinaweza kusaidia kuwainua wananchi wa huko? Kama chadema ndo kina sera zinazoweza saidia kuleta maendeleo huko kwa nini usianze wewe kuwaelimisha wananchi wa huko wakifahamu na kukiunga mkono ifikapo 2015.
 

No PROBLEM -- You can be an ENEMY WITHIN.. Mfano Mzuri ni Democratic Party USA... ni GROUP KUBWA sababu ajenda za DEMOCRATIC PARTY ni NYINGI sio wote wanakubaliana na AJENDA ZOTE sasa kuna wengine wameshinda Maeneo ya REPUBLICANS na karibia 80% wanaVOTE with Republicans lakini kichama ni DEMOCRATS...

Kama utagombea kama CCM lakini AJENDA zako bado SI ZA KIFISADI... More POWER 2 U..
 
Mkuu sidhani kama kuna aja yakuomba ushauri,soma alama za nyakati ksha chukua hatua.kama unataka kuikomboa tanganyika kutoka mikononi mwa wakoroni weusi kuwa namsimamo. kama unataka kuchumia tumbo wasikilize wazee
 
kwa kuwa wanaonekana kukuamin jaribu kuwaelewesha kama ubora wa kiongozi sio chama bali ni uwezo wa mgombea bila kuangalia chama alichopo. lakin kitu cha pili waelimishe kuhusu sera za Cdm zilivyo nzuri na bora kwa maendeleo ya wanasame.
 
na kama vijana nao wakikushauri vingine utafanyaje? akina mama nao je! mbona unataka kuwatumia wazee kama kichaka cha kujifichia ndugu? cha msingi ni jinsi gani utasaidia kutatua kero zao!
 

Wewe huna tofauti na ndumi la kuwili na watu wa aina kama ulivyo mguu ndani mguu nje ni wasaliti vile vile una tamaa kama ile iliyomponza fisi...
 
Fuata ushauri wa wazee. Na Same Magharibi, CHADEMA haipo kabisa...
Wewe unataka ubunge au kuwatumikia wananchi? Kama unataka ubunge fanya kama wazee walivyokushauri ila uwe na pesa za kutosha kwani utauziwa ubunge. Kama unataka kuwatumikia wananchi pitia cdm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…