Mkuu.@Njaa Nenda hopitali kuu ya Muhimbili hapo Mjini Dar kama upo hapo.La kama haupo hapo nenda hospitali kubwa unapoishi wewe usidharau hayo matatizo yasije baadae yakawa ni makubwa uwe muangalifu.
Sijawahi kusikia allergic reaction ya aina hio nadhani una mtatizo mengine au inflammation ya kawaida tu nakushauri uwahi hospitali uchukuliwe ultrasound ya koo lako na vipimo vya hayo maugali na TSH/FH4 ikiwezekana ili kuhakikisha hauna GOITER! Mueleze daktari kuhusiana na hayo "maugali" yanayotoka kooni!Habari zenu wakuu....
Nimekuwa na maumivu ya koo kwa muda fulani, maumivu sio makali ila huwa nahisi kama kuna kitu kinakwaruza na kuuma kiasi (kwa muda mrefu sasa). Tatizo hili hutokea mara kwa mara hasa ninapokaa chini kwa muda mrefu kuandika. Nimeenda kwa madaktari mara kadhaa na huwa naambiwa kuwa kuna inflammation (kuvimba). Nilipouliza sababu wakasema mara nyingi ni aleji au matumizi ya vitu baridi... Niliamua kuacha vitu baridi ila bado hali hii hujitokeza...
Siku za hivi karibuni nimekuwa nikitoa vitu vya ajabu kooni, vinakuwa kama vipande vya ugali (saizi ya punje za mahindi) vyenye harufu mbaya sana, wakati mwingine nikikohoa tu vinatoka. Nilipewa dawa vikapungua......, Wiki hii nilihisi kuna kitu kinakwama kooni, nikaamua kuingiza vidole na kutoa hayo maugali kisha nikajisikia vizuri kabisa! Ila inaniogopesha sana ingawa mtu fulani akaniambia ni vitu vya kawaida......
Naomba ushauri na uzoefu wa hili? Je ni dalili ya nini? Mbona madaktari wanalichukulia poa? Ikiwezekan ni-PM
Nawakilisha
pole mkuu nlivyoelewa hilo tatizo lako linaweza kuwa una
1. diverticulum... hili ni tatizo la misuli kulegea na kutengeneza mfuko wa pembeni (out pouching) kwa eneo kama hilo inaitwa zenker's diverticulum ... ndo maana vyakula vinaingia hapo badala ya kwenda tumboni
UCHUNGUZI na vpimo... kwanza wanafanya barrium swallow x-ray itaonyesha mfuko pili uanweza kufanya endoscope... nenda muhimbili.... kama ungekuwa mwanza ngekuona.
MATIBABU... ni upasuaji hakuna dawa ya kuondoa tatizo.
ingawa hili tatizo huwapta wazee but rarely kwa vijana pia
2. inaweza kuwa uvimbe kama tonsilitis,adanitis, jipu.. goitre au benign tumor not cancer usiogope... vyote hivi mpaka upasuaji fanya vile vipimo vya hapo juu