Kiwanja hiki kinaukubwa sawa na uwanja wa mpira wa miguu ( a standard football pitch/ground)...kipo barabarani eneo la madale dsm na linafaa sana kwa petrol station maana sehemu ile hamna(sio lazima ni pendekezo langu). Bei ni tzs milioni 100.
Kiwanja hiki kinaukubwa sawa na uwanja wa mpira wa miguu ( a standard football pitch/ground)...kipo barabarani eneo la madale dsm na linafaa sana kwa petrol station maana sehemu ile hamna(sio lazima ni pendekezo langu). Bei ni tzs milioni 100.
Hii nadharia watanzania wanazidi kunivunja mbavu kila kukicha. Kiwanja hicho kwa bei hiyo hata kingekuwa katikati ya jiji bado kungekuwa na mabishano ya bei, sasa huko Madale nawe kutoa pendekezo la kufanya Gas station siona mantiki yake.
Urahisi wa kujipangia pesa kama hizo kwa wauza mirungi hana uchungu na pesa yao, lakini mvuja jasho atajuliza mara mbili pesa alizotaabikia.
Kiwanja kina hati halali ya mmiliki na mawasiliano nimeweka kwa muhitaji ambaye yupo serious...kuhusu matumizi ya kiwanja nimeeleza awali kuwa ni maoni yangu na siyo lazima kwani ni kama ununue suti alafu muuza duka akushauri uivae siku ya harusi na wakati wewe unaweza kuiona inafaa kwa kunywea bia weekend na sio harusini...Kuhusu bei mimi naona ni ya kawaida kwani kama mtu anaweza kujinunulia land cruiser V8 kwa gharama kubwa unadhani anashindwa kununua uwanja kama huo akainvest watu kadhaa wakapata ajira juu yake na familia zao zikamuombea aendelee kuishi duniani maana anawasaidia...thanx
milion 100 na petrol station...mnhhhhhhh...ngoja nikutumie namba za jamaa yangu mohamed barhboob, oilcom, felix mosha, riz-1 na wadau wengine kwenye biashara ya mafuta...ila kama unaongelea 10m na kushuka chini sisi ndio wateja wako..au vip????