Bado kipo wakuu... Karibuni.Nauza kiwanja kinachopatikana Itezi Mbeya.
SIFA ZA KIWANJA
1. Kimepimwa na hati ipo.
2. Umeme hauhitaji nguzo au nguzo moja ukihitaji.
3. Nimeweka msingi wa mawe wa nyumba (Trip 9).
4. Mashimo mawili ya choo yameshajengwa kabisa (Kubwa la mawe na dogo la tofali za block).
5. Kina ukubwa wa Sqm 650.
6. Ramani iliyokuwa inajengwa nitaitoa kwa mnunuzi kama akipenda kuendeleza.
MUUZAJI
Ni mimi mwenyewe, hakina dalali.
MAWASILIANO
0710613913 (Calls Only)
0764615124 (Calls na WhatsApp)
SABABU ZA KUUZA
Nimehama kimakazi Mbeya.
GHARAMA
Kiwanja pamoja na vitu vilivyofanyika ni Tsh 10m.
Kuona kiwanja ni bure kabisa.
Karibuni sana.
Thubutu, maneno mengi utafikiria anauza Banghe!Weka picha acha maneno mengi
Ni Itezi Mashariki ama Magharibi?Sawa mkuu
Wakuu hizi picha za leo za eneo kwa mliohitaji kwa simu nimewatumia na wengine karibuni mtathimini eneo.
Kwa video nichek whatsapp nikutumie nashindwa kuipandisha hapa.View attachment 1908167View attachment 1908168View attachment 1908170View attachment 1908173
Si unajuwa tena Mbeya barabara za mitaa ni mbovu ama kwingine hakuna, atauza tu, awe mvumilivuDuh tangu February hadi Leo hujauza?
Nadhani changamoto inaweza kuwa ule msingi wa nyumba ambao tayari upo, pengine wanunuaji wanakua na idea ya aina ya nyumba wanataka kujenga. Hivyo kuwepo kwa msingi ni kama kikwazo. Itakubidi ufanye modification kidogo kuendana na idea yako- which can be costly.Duh tangu February hadi Leo hujauza?
Thanks mkuuNadhani changamoto inaweza kuwa ule msingi wa nyumba ambao tayari upo, pengine wanunuaji wanakua na idea ya aina ya nyumba wanataka kujenga. Hivyo kuwepo kwa msingi ni kama kikwazo. Itakubidi ufanye modification kidogo kuendana na idea yako- which can be costly.
Pia 10M kwa maeneo ya Itezi nadhani vitu ambavyo ameshafanya kwenye plot ndio vime'inflate bei kiasi. Naamini atapata mteja sababu Plot ya 650sqm ni size nzuri sana kwa makazi.
negotiate mzee. usihofuIngekuwa kwenye 4-5.5M nungejitosa walau nipajenge kidogo kidogo, ila 10M naishia kusoma tangazo na kuishia kugugumia tu...