ndandawamalenja
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 548
- 661
dah! maajabu kweli kweli.
anyway nijuavyo mm hata kwenye tafiti device yoyote ile utakayoitumia lazima uitaje na usema kiko calibrated kwa kiwango gani na kimetengenezwa wapi. sasa ndugu yangu mtoa mada kama alitumia stethoscope ama alitumia darubini sisi hatuwez kujua inatakiwa utuambie ni kidude / mashine gani alitumia.
Yaani my dear gfsonwin siku hizi kumeibuka mambo sijui yanatoka wapi na serikali yetu kimyaaaa! Anchosema mtoa mada ni kama ile wanayoita kupimwa mwili mzima unaambiwa magonjwa kibao in the end wanakwambia dawa tunayo hapa na utaona sio dawa bali unapewa suppliments.... Imesambaa kila mahali watu wanaibiwa pesa zao utakuta mtu ana high blood pressure anaacha dawa za hospitali utamuona siku anakuja na stroke unaambiwa alikuwa anatumia dawa ukisoma zote ni suppliments wanazokuonyesha...
Haya bana/Jamani mimi nina mtu alikuwa anasumbuliwa na tatizo la low blood pressure,akapimwa kwenye hospital moja kubwa tu hapa jijini ikaonekana ana tatizo la cholesterol nyingi,akaenda kwa hao jamaa wa tiba mbadala na kuchekiwa kwa hicho kipimo alichokisimulia- ndandawamalenja ikaonekana ana tatizo hilohilo la Cholesterol ila kipimo kiko more detailed kwani kinaonyesha na viwango vya madhara,alipewa dawa ndani ya wiki mbili ile hali ikaondoka kwa almost 50% na ndani ya mwezi akawa fiti sana na alipokwenda kucheck hospital ilionekana hana tatizo tena la cholesterol,pia alipo check na hawa wa tiba mbadala ikaonekana tatizo limeisha,jamaa ana zaidi ya mwaka sasa yuko fiti.-
Hili Swali halikupata jibu muafaka, wataala tupeni majibu maana hivisasa hivyo vipimo vimeenea sana. MziziMkavu Kiranga gfsonwin measkron SnipperHivi majuzi nilienda kwenye kituo kimoja cha tiba mbadala, pale Mbezi beach. Kinaitwa Fadhaget Sanitarium. Dr. akanipa kidude kidude flani hivi nishike kimeunganishwa na computer, akaclick kinini sijui kikaanza kufanya kama kinascan viungo muhimu vya mwili. Ubongo, moyo, figo, mapafu, etc. Huku kinadisplay activities na information kwenye screen ya laptop. Baada ya dakika 2 hivi kikamaliza na kutoa report. Dr akaanza kunielezea sasa, lakini alichofanya ni kunichanganya tu kwa sababu nikawaza kwamba kile kimachine ni geresha tu. Kwamba kama kupima afya ya mtu ni rahisi hivo, inakuwaje tunapopima mahospitali makubwa kabisa inachukua muda sana, mpaka wakutoe damu kibao na mambo mengine halafu kahospitali kadogo tu kanatechnolojia ya kupima mwili wote kwa sekunde sitini? Hivi hii sio program ya kutuibia ambayo inatoa majibu yaleyale but randomly kutokana na watu mnavyokuja? Naomba wataalam mnifumbue macho!!