Kinywa Cha mpumbavu

ndayilagije

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Posts
7,490
Reaction score
8,305
Wapendwa mbarikiwe na Bwana.
Leo ni ijumaa kuu,na jamii your ya wakristo duniani wanaadhimisha mateso ya Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo.Tunapoendelea kutakiana amani ninawiwa kuwa kumbusha kuhusu kinywa Cha mpumbavu.(Mithali 18:7)
Yumkini umeumizwa,umedhulumiwa,umeonewa au kudharauliwa. Nikutie moyo kwa neno hilo.Na nikukumbushe tu kuwa hakuna lidumulo chini ya jua.
Yote unayopitia yatakoma siku na saa usiyoijua na si kwa kupiga kelele.
Dunia ni nzito sana hata Yesu alikiri kuiona dhiki ulimwenguni.
Kama ningeeleweka vema ningetamani kila mtu akae kimya tu,asiseme jema Wala baya alionalo...lakini najua haiwezekani.
Amin,Amin nakuambia hata akusononeshaye hana furaha kama unavyodhani.
Nwatakie sikukuu njema na Mungu akayaone machozi yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…