King'amuzi cha startimes ifakara

Naipuli

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2012
Posts
266
Reaction score
110
Habari waungwana wa JF.
Ningependa kujuzwa kutoka kwa mwenye ujuzi wa hili.
Awali nilikuwa Dodoma na nilikuwa natumia King'amuzi cha StarTimes, sasa nimehamia Ifakara, Kilombero, Morogoro; lakini nikiunganisha King'amuzi sipati Channel yoyote.
Kinachonishangaza zaidi nikipita kwenye baadhi ya maduka nakuta wamejaza hizi Decoder za ST kibao zinauzwa na nilipouliza kama zinafanya kazi muuzaji alinambia ndio, lakini mimi kwangu ndo kama hivyo.
Je, ni kweli vinafanya kazi huku niliko?
Kama jibu ni ndiyo; Mbona kwangu kinagoma, tatizo laweza kuwa ni nini? NISAIDIENI.
Kama jibu ni hapana; Mnanishauri nifanye nini?
MSAADA WENU TAFADHARI.
 
startime haipatikan ifakara kwa hakuna mnara wowete uliokwisha jengwa huko.
 
Jaribu zuku au dstv, unapata signal zao through satelite, hii itamaliza tatizo la eneo ulilopo na hata ukienda mkoa mwingine ni suala la kutafuta fundi wa kufunga dish zao tu!
 
Ving'amuzi vya startimes dodoma n Dvb T1 havifany kaz kabsa Morogoro ...hapa tunatumia Dvb T2
 
Mkuu Naipuli unakaa kwa jongo,viwanja sitini,maendeleo,michenga au mbasa?
 
Last edited by a moderator:
Ving'amuzi vya startimes dodoma n Dvb T1 havifany kaz kabsa Morogoro ...hapa tunatumia Dvb T2

DVB T2 ni vya StarTimes pia au ni wengine?
If yes, navipataje hivyo vya DVB T2?
 
DVB T2 ni vya StarTimes pia au ni wengine?
If yes, navipataje hivyo vya DVB T2?

N hiv vya startimes, DVB T2 ndo ving'amuzi vinavyo uzwa Moro,vina alama ya DVB T2 kwa mbele na vinapatikana ofsn kwao hapa Moro town
 
Ifakara ni mbali sana kutoka moro mjini ,nakushauri kabla ya kununua hicho king'amuzi cha Dvb T2 fanya utafiti kwa kuuliza watu wengine hapo iwapo wanapata startimes. Kama mikumi na kilombero sikuona watumiaji wa startimes na wao wapo karibu na moro je inawezekana kwa ifakara iliyo mbali?
 
ifakara hakuna star time ila zuku dstv na local na hivyo ving'amuzi ulivyoviona dukani siyo vya star time........
 
DVB T2 ni vya StarTimes pia au ni wengine?
If yes, navipataje hivyo vya DVB T2?
Unawapelekea hicho wanakupa kingine, ilinipata mie dar to zenji,nilienda wakanibadilishia kutoka DVB T1 to DVB T2 sasa poa kabisa!ila wanakulazimisha ulipie package ya 10,000 kwa miezi sita ,20000 kwa miezi mitatu, au ya 40000 for almost 2 month( as they calculate any package from 59000 which you must pay for swaping)
 
Nashukuru sana wadau kwa maelezo yenu, kwa hakika nimeelewa vema.
Kwahiyo mnanishauri nitumie nini kati ya hivi:
1. Dishi, aina gani ya dish na receiver yake.
2. King'amuzi cha Zuku.

Natanguliza shukurani zangu kwenu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…