Kimya Kimya Lakini Wamekuja

MUTTAZ

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2016
Posts
296
Reaction score
237
Katika siku, week na miezi ya hivi karibuni Tanzania tumebahatika kutembelewa na MaCelebrity wengi, ndio nasema wengi kwani hapo kabla ilikuwa nadra sana kutembelewa na jamii hii ya watu maarufu nchini hasa katika nyanja ya Utalii. Kwa mfano katika kipindi kisichopungua miezi miwili tumetembelewa na;
  • Harrison Ford;
  • Usher Raymond;
  • Mamadou Sakho nad his family;
  • David Beckham and his family;
  • Everton Team na;
  • Tottenham Hotspur midfielder Christian Eriksen!;
  • Nahodha wa timu ya Simba, Jonas Mkude akiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane, Mwanza;
  • Morgan Schneiderlin inasemekana msela huyu alikuja kwa fungate na mkewe!;
  • Tottenham Hotspur midfielder Kenyan International Victor Wanyama licha ya Mtaa wake kung'olewa kwa hisia nyeti za kisiasa!;
  • Na wengine walionitoka kwa kichwa!
Hoja yangu, nikwa kiasi gani Wizara ya Habari na wizara ya Utalii imetumia vyema fursa hii kwa ajili ya kuongeza Idadi ya watu wa namna hii kuja nchini? Je, wameondoka na kuk=mbukumbu yeyote nzuri ambayo itawafanya wawe mifa rasmi na mabalozi wema wa nchi yetu na waweze kuja siku nyingine kuitembelea Tanzania ambayo siyo rahisi kumaliza vivutio vyake vyote kuvitembelea kwa muda wa week?

Ninaamini fika kabla ya hawa watu wa jamii hii ya kicelebrity kufika nchini mwetu lazima serikali huwa inataarifa muhimu za ujio wao, je huwa serikali inajiandaa kuwatumia hawa watu punde inapopata taarifa za ujio wao, binafsi ninaamini kama tungekuwa tumejipanga kwa ujio wa hawa jamaa basi tungaliweza kutumia gharama kidogo sana kwa ajili ya kujitangaza kupitia hawa jamaa na mwisho wa siku kuingiza fedha lundo nchini kwa ajili ya ku finance budget ya taifa.

Kwa mfano, majuzi tulikuwa na akina Rooney! Hawa jamaa wataondoka na nini kukipeleka huko makwao na hasa kwa wenzao wa EPL?

Je licha yakuja kimyakimya na wachache wao ikiwa sio kimya kimya na sisi tumewapokea na kuwaaga kimyakimya?

Jamani naomba kuwasilisha na karibuni sana!
 
Ni hatua nzuri sana kwa maendeleo ya utalii wa nchi yetu...
 
Mgeni njoo mwenyeji APONE.
Mgeni njoo mwenyeji AKOME.
.
[HASHTAG]#WAHENGA[/HASHTAG]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…