Kimenuka mwibara/Bunda

Sexer

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Posts
8,504
Reaction score
8,253
Wakuu ccm inakata roho kwa tabu sana labda sijui kwa sababu ya madhambi iliyotenda?! Katika jimbo la mwibara kangi aliwanunua washindi wa pili, tatu,nk ktk kura za maoni za udiwani chadema pamoja na viongozi wa chadema wa eneo hilo ili wagombea hao walioshindwa wakachukue form ya kugombea udiwani, cha ajabu mkurugenzi kawapa form lakin kilichotokea ni shida! Makanda wamekinukisha hadi ikabidi wagombea halisi ndo wapewe form na wale mamluki kutenguliwa. Kipindi wanachonga huo mchongo wao kama kawaida makamanda walikuwa wanawachora tu na hako kamchezo kao wakarekodi hadi clip za video ambazo zilitumwa makao makuu ya chama nacho chama kimeshachua hatua kimewaengua karibia viongozi wa eneo hilo.
Kasheshe lingine lilikuwa pale bunda, katika hali ya kushangaza na kutia aibu makada wa ccm walienda kwa mkurugenzi kuzuia esther bulaya asipewe form ya kugombea ubunge, madai yao eti kwa nini apewe aliyeshika nafasi ya tatu aachwe wa kwanza?! Aisee palichimbika kwelikweli pamoja na kwamba aliyeshika namba 1 alikuwepo pale na alisisitiza wao chadema ndo wameamua hivyo sasa wao ccm kinawauma nini?! Lakin maccm yaliendelea kukomaa hadi ikabidu waitwe wanasheria kuja kufafanua hayo mambo kisheria ndipo maccm yakanywea na Esther akachukua form.
 
CCM wanapenda sana kuingilia mambo yasiyowahusu.

Mwaka huu ndio mwisho wapi.
 
Mkuu tunashukuru kwa taarifa hizo za ukombozi wa nchi yetu,vipi hapo bunda mjini kamanda bulaya anakubalika?
 
Team madodoki bwana hata wanachoandika hakieleweki, vipi kwanza kazi ya kumuogesha fisadi imefikia wapi?
 
duh hao hawana hata aibu, bulaya anamchinja wasira asubuhi na mapema tar 25
 
Bunda ndio kwa wassira? Kama ndio basi apigwe tu tena apewe kipigo cha aibu
 
Mkuu tunashukuru kwa taarifa hizo za ukombozi wa nchi yetu,vipi hapo bunda mjini kamanda bulaya anakubalika?

Kwa jimbo la Bunda mjini, Esther Bulaya ndio habari ya mujini, namsikitia mzee wetu namna alivyojitahidi kuchakachua kwenye kura za maoni mpaka akapita halafu anakuja kukutana na kisiki! Cjui atapona au ndio kumpoteza kwa Pressure?
 
Hii tabia ya kuendekeza siasa za kueneza uchochezi, kashfa, chuki na matusi haiwasaidii na kamwe haitowaidia kitu. Kaeni mkijua kuwa nyie na familia zenu na koo zenu hamna immunity ya madhara yatokanayo na tabia kama hizi za kwenu. Hii ni nchi ya watanzani na sisi wote ni watanzania hakuna maukawa wala maccm.
 
Mkuu tunashukuru kwa taarifa hizo za ukombozi wa nchi yetu,vipi hapo bunda mjini kamanda bulaya anakubalika?

Mkuu hapa bunda bulaya anakubalika mno, yaani hata angegombea kwa ccm angetushinda chadema, nashukuru ccm kwa kumuwekea mizengwe mapema nae bila ajizi akajiunga nasi, atashinda asubuhi tu
 
Bila shaka unawaambia wale makada waliotumwa na wasira kumzuia bulaya kuchukua form?! Ni vema umewaeleza
 
Kwa jimbo la Bunda mjini, Esther Bulaya ndio habari ya mujini, namsikitia mzee wetu namna alivyojitahidi kuchakachua kwenye kura za maoni mpaka akapita halafu anakuja kukutana na kisiki! Cjui atapona au ndio kumpoteza kwa Pressure?

Mkuu huyo Mzee ni kumzoa kwa kimbunga bila kumuangalia usoni maana unaweza kumuonea huruma
 
Mkuu hapa bunda bulaya anakubalika mno, yaani hata angegombea kwa ccm angetushinda chadema, nashukuru ccm kwa kumuwekea mizengwe mapema nae bila ajizi akajiunga nasi, atashinda asubuhi tu

Asante sana kwa kutuletea chakula ya ubongo mkuu,huu ni mwaka wa maamuzi na tunahitaji rais lowasa awe na wabunge wakutosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…