Palipo na mnyarwanda, mkenya yupo nyuma yake. Ona sasa hii..
Maziku Masunga Jr. Tatizo lenu kubwa ni unafiki, na ndio maana hata mkisema na kumtaja Kagame kivipi inakua gumu kuaminika au kuskilizwa. Nyie hapa mpo kutwa mnajadili nchi za watu, mnaandika kuhusu Marekani, Urusi, Syria, Burundi, Kenya, Rwanda n.k. lakini nchi yenu ikitajwa tu, mnatiririka kwa povu eti tusiongelee kuhusu Tanzania. Huo ni ubinafsi, uroho na unafiki uliopitiliza.
Nyie sio malaika, kama nilivyosema kwenye mada nyingine sehemu, ujamaa uliwaadhiri na kuwafanya kuwa introvert. Hamtaki kutoka, hamtaki kuendana na yeyote, hamtaki yeyote aongee kuwahusu, lakini mpo radhi kuongea chochote kuhusu nchi za watu wengine. Nimeishi na nyie na ninawafahamu kabisa, hampo malaika hata kidogo na mna mapungufu kama binadamu wengine.
Na kwa vile nchi yenu ipo hapa duniani kwenye hizi enzi za globalization, mtatajwa tu iwe kwa mabaya au mazuri, magazeti yataandika kuwahusu, mada zitaanzishwa kuwajadili, mtameza na kutema lakini tutaandika tu hadi mtazoea kuishi na binadamu kutoka nchi zingine.....huwa napata raha jinsi mnatiririka kwa povu nikiweka mada kuhusu Tanzania. Sio kwamba naichukia nchi yenu, lakini matusi yenu ndio huwa yananipa raha na kuonyesha kuwa taratibu mnafunguka into the global village.