Pamoja na mapungufu yaliyo ndani ya CCM, wananchi wa Tanzania tunalazimika kukimbilia huko kwa kuwa wapinzani wametusaliti. Haiingii akilini, miaka zaidi ya ishirini, upinzani hawana hata mtu mwenye sifa ya kugombea uraisi hadi wamsimamishe aliyekataliwa na CCM tena kwa kashfa. Cha kusikitisha ni kwamba, si tu aliyesimamishwa kwa ticket ya UKAWA alikuwa ni mtuhumiwa namba moja wa wizi serikalini (kwa mujibu wa CHADEMA), pia hata uteuaji wake kugombea uraisi haukufuata utaratibu wa kidemokrasia, kitu ambacho kiliwaacha Watanzania wengi midomo wazi wakijiuliza "inakuwaje mtu anajiunga leo na chama, halafu kesho yake anagombea uraisi". Kwa mwendo huu, hatuna budi kuwaunga mkono CCM maana walau wana utaratibu ambao usipofuatwa, unaweza kwenda mahali na kuulalamikia, ndani ya chama. Lazima tukubali ukweli, wapinzani wanafanya mambo kiholela na hili ni tatizo kubwa saana kwa taifa. Leo hii wapinzani walichonacho hata hakina jina, maana UKAWA walianza kama mwamvuli wa kupigania Katiba ya wananchi, lakini kwa sasa hata sijui wanachofanya ni nini. Labda wewe mpinzani tusaidie.