Kidogo Kuhusu NCCR-Mageuzi

Nicolas J Clinton Gabone

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2014
Posts
897
Reaction score
559
KIDOGO LEO KUHUSU HARAKATI ZA MAGEUZI NA NCCR-Mageuzi

Kwa Hisani ya Bubelwa Kaiza.

."...ilitosha kuelewa kwamba Watanzania waliojitolea kuasisi Mageuzi ya demokrasia ya siasa za ushindani wa vyama wangekwama kwa kukosa pesa za kutekeleza mipango yao.

Hata hivyo, mapungufu katika kutekeleza sera za kujenga Tanzania iliyofuata sera za Kijamaa au Ki-Socialist, uliwezesha baadhi ya Watanzania kupata fursa ya kuwa na mapato kidogo ya ziada, mitaji ya kifedha na hata mitaji ya kijamii. Miongoni mwa Watanzania hao ndio waliosaidia Kamati ya Mageuzi (NCCR) kuweza kutekeleza shughuli zake. Licha ya kuwa viongozi wa Kamati; Dk. Ringo Willy Tenga, Ndimara Tegambwage na Prince Mahinja Bagenda walitoa misaada mikubwa ya kifedha kusaidia Kamati (NCCR) kutekeleza mipango yake.

Kuna watu wengine waliochangia Kamati ya Mageuzi (NCCR) Mzee John Kolos Kapinga (aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa shirika la uchumi la Chama Cha Mapinduzi (SUKITA); Bwana Bruno Mpangala, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA); Bwana Reginald Abraham Mengi aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP; Bwana Joseph Mungai, aliyewahi kuwa Waziri wa Elimu na Utamaduni; Bwana Christopher Gachuma, mfanyabiashara na mmiliki wa kampuni ya Nyanza Botllers; Bwana Emmanuel Makubo, mfanyabiasha wa jijini Dar es Salaam; Bwana Gibson Balyagati, mfanyabiashara wa jijini Dar es Salaam; Mzee Alex Khalid, mmiliki wa Makondeko Holdings; Mzee Edward Barongo na wengine wengi.

Aidha, ujio wa Mageuzi ulitoa fursa kwa viongozi na watendaji ndani ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali kutathmini nafasi walizokuwa nazo, kuweka matumaini ya kupanda ngazi za madaraka na kuanza kuweka ndoana zao kwenye Mageuzi. Mzee Samuel Sitta, wakati huo akiwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, alikuwa na matumani ya kupanda ngazi ya madaraka kupitia Mageuzi. Licha ya kuonekana mwoga, Mzee Samuel Sitta alikuwa akienda Dar es Salaam akifanya miadi na mikutano ya siri na viongozi wa Kamati ya Mageuzi huku akieleza nia yake ya kupewa fursa ya kugombea urais kupitia upinzani. Hakufanikiwa kutimiza ndoto yake."

NCCR-Mageuzi ni juhudi za Watanzania wenyewe kujikusanya ili kuleta ushawishi na ushindani wa kisiasa na kidemokrasia Nchini katika sera, itikadi na falsafa.

Nicolas J Clinton,
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Mageuzi (JUVIMA)- NCCR-Mageuzi.
​
 
NCCR-MAGEUZI ya kipindi hicho ilionekana inanguvu, ushawishi na tumaini kwa wengi, sio hii ya sasa haina mvuto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…