Ndugu zangu,
Mimi sio mtu wa hotuba ndefu zisizo na mashiko na wala sipendi kumchosha mtu na waraka mrefu usio na tija.
Kwa leo ninaomba kupata majibu ya maswali yangu haya;
1. Mh Godbless Lema yupo gerezani kwa kesi ya kuelezea maono kwamba ameoteshwa ikiwa Raisi wa Tanzania hatajirekebisha na kuthamini mchango wa wapinzani na pia asipende kujiona mungumtu basi haitafika 2020 MUNGU mkuu atakuwa amechukua uhai wake.
Je, kama hii ndoto ikatimia na lema akiwa bado gerezani atafunguliwa kesi ya (a)mauaji? (b)atahukumiwa maisha kwa utabiri wa kifo?
1. Baada ya Mh lema kufikishwa mahakamani ilionekana kuwa kesi hiyo ina dhamana na mh hakimu aliyesikiliza kesi aliona dhamana iko wazi lkn baadae baada ya kwenda mapumziko na kurudi ikaonekana kesi haina dhamana,je hakimu mapumziko aliweza kupata ushauri tofauti?je kama alipata ushauri tofauti kuna sababu ya mahakimu kula kiapo?
2. Tunajua mahakama zetu ni huru na haziinguliwi ingawa sio wote wanaoamini hivyo,inawezekana mh lema akawa alifanya kosa kutoa maono yake hadharani,mh lowasa alitabiriwa kufa mara moja baada ya uchaguzi na waliomtabiria mbona hakuna hata mmoja aliyekamatwa au kufunguliwa mashtaka?jibu ikiwa kwamba lowasa alikuwa mgombea tu na si raisi hivyo kutabiriwa kwake hakuna shida,je kwa MUNGU neno kufa lina urais au kapuku?
Mwisho
Tujifunze kupendana,hasa ni wajibu wa mzazi kumuonyesha mtoto upendo,kama mzazi wewe kila ukirudi ndani ni hasira na matusi na ubabe kwa wanao usitegemee kuheshimiwa ukiwapa kisogo wanao lazima wakutukane na kukung'ong'a maana hakuna wanaloliona jema kwako.
Tupendane kukomoana hakutajenga na mbaya au nzuri zaidi wote tutakufa uwe tajiri uwe masikini uwe mbunge uwe rais wote tutaliwa na funza.
"Dunia ya MUNGU,vitu ni vya mzungu".
Swelana.