Ikiwa tunakubaliana kuwa muda wa maandalizi hautoshi kwa Katiba mpya kutumika uchaguzi wa 2015 basi la muhimu ni kuweka mazingira ya kufanyika uchaguzi huru kwa katiba tuliyonayo. Tatizo Tume huru itaundwaje katika mzingira haya? Sidhani kama uteuzi wa wajumbe tu kutoka taasisi malimbali utaifanya tume hiyo kuwa huru. Hilo la pili (kuongeza muda) tumeshaanza kusikia tetesi, lakini sidhani kama litapitishwa, upepo unavyovuma ndani ya Chama na nje wanaonekana kusubiri 2015 kwa hamu kubwa, ikiwemo na ya uchu mkubwa.Ahsante mtoa mada(Getstart) hapojuu. Hapa nionavyo mm ni kwamba kwa kujua au kutojua mazingira yanatengenezeka ya serikali iliyopo kutofikia kikomo 2015 au kuharibika kwa vyote viwili; katiba mpya na uchaguzi mkuuHivo basi tufanye mawili yafuatayo1. Tuandae mazingira ya kufanya uchaguzi huru na wa haki katika spirit safi kabisa ya kuwa na serikali halali (legitimate government) kwa kuandaa mazingira ie kuundwa Tume Huru ya uchaguzi...tukiwa bado chini ya katiba hii tunayoenda nayo. Hili linawezekana maana political and social atmosphere iliyoko ss ni ya kufanya mageuzi katika jinsi ya tunavofanya mambo yetu kama taifa. Uchaguzi ufanyike chini ya katiba hii, tumalize uchaguzi tuanze kuandaa mazingira ya kuimplement katiba mpya.Tujipe muda, tufanye jambo moja at a time maana demokrasia yetu bado changa na ss hv iko volatile. Tukiyachanganya haya mawili ya uchaguzi na katiba mpya tutayaaribu yote. Ni muhimu yote mawili yafanikiwe kwa kiasi kikubwa sana. Kuyachanganya kunaweza kwa haraka tu ku-politisize mchakato wa katiba na hivo kuuharibu kabisa. Consequencies za hali hiyo sina haja ya kuzieleza; ziko wazi vizazi kwa vizazi vijavyo.2. Ni kujitayarisha kuona serikali iliyopo inaendelea kutawala zaidi ya kikomo chake (2015) ili tupate katiba mpya, tuandae mazingiya ya kimifumo halafu ndo tufanye uchaguzi.Hili la pili silipendi lakini madhara yake si makubwa kama kuyachanganya mawili kwa muda mmoja isipokuwa tu litaweka precidency mbaya.
Mchmlay unafikirti tume huru inawezekana kwa kuhusisha asasi mbalimbali bila kubadili katiba?Kusema ukweli na bila kutafuna maneno ni kwamba kama tunataka katiba nzuri na ya kudumu itakayoisaidia nchi hii kwa miaka mingi, muda uliobaki utakuwa hautoshi. Kutokana na hali hiyo mimi ningependekeza mambo machache kama ifuatavyo:1. Kwamba, kwa ajili ya kuepuka vurugu na malalamiko kutoka kwa watu wengi, uchaguzi ujao ufanyiwe marekebisho ambayo yatawezesha kufanyika kwa uchaguzi huru.2. Kwa hiyo, tume ya uchaguzi ambayo ndiyo imekuwa ikilalamikiwa zaidi ifanyiwe marekebisho makubwa. Yaani ni kwamba, iundwe tume huru kabisa na ambayo muundo wake utatokana na asasi mbalimbali za kiraia, taasisi mbalimbali za kidini na NGOS. Tume hii iwe completely free na isiingiliwe kabisa na mfumo wowote wa serikali