Wana JF nafikiria kuanzisha kampuni ya usafirishaji wa mizigo. Natarajia kupata mshiko wa kutosha kununua malori used semi trailers 3 au 4, je hili ni wazo zuri? natamani kufanya hii shughuli inanivutia sana lakini sina uzoefu nayo na sijui kama inalipa au vipi, naomba mwenye mwanga aniangazie kidogo bila dhihaka tafadhali.
Mimi ni transporter nipo kwenye hii field mda mrefu! Kazi inalipa ikiwa utapata contract ya mda mrefu otherwise inaumiza kichwa, running cost ni kubwa! Anyways karibu
karibu sana nami niko sekta hii kwa muda mrefu tangu nikiwa dereva,afisa wa usafirishaji hatimaye kuwa mmiliki,kazi inalipa kama utapata mkataba etc kama mimi nimepata mkataba WFP,shida nyingine drivers wengi sio waaminifu,karibu sana

Karibu mimi pia nipo kwenye hii biashara. Kama utaisimamia mwenyewe ni biashara nzuri. Madereva asilimia kubwa sio waaminifu. Sisi wasafirishaji wadogowadogo kama tungepata njia ya kushirikiana ni rahisi kupata mikataba lakini ni kazi sana sisi kushirikiana.

Sisi wasafirishaji wadogo wadogo tunaweza kushirikiana lakini lazima iwe wazi tunashirikiana kwenye maeneo yapi, ili kila mmoja aweze kulinda interest zake, tunaweza kuanzisha ofisi ya umoja wa washafirishaji wadogo wadogo yenye makusudi ya kuratibu baina ya wateja na wasafirishaji, yaani inapokea maombi kutoka kwa wateja na kuyapeleka kwa kampuni za usafirishaji ambazo ziko ndani ya umoja. Hii ofisi itakuwa inakuja kampuni gani ina tenda na ipi haina
Asante kwa majibu mazuri. Jee nini jawabu la hawa madereva ambao sio waaminifu? Mimi nimeingia kwenye hii biashara mpaka sasa nafikiria kuiacha. Wenzetu mnafanyaje na hawa madereva?