Kwa kiasi fulani, pengine kiasi kidogo CCM ni sababu tosha ya hali ngumu ya maisha, kiasi kikubwa nionavyo mimi ni sisi wananchi. We are not doing enough for ourselves, we cheat too much on almost everything, tunaiba, kuhonga na kuhongwa rushwa katika kila nyanja, kazi hatuifanyi vile ipasavyo, tunalalamikia wengine as if wao wamezaliwa kuishi kwa niaba yetu au tumezaliwa tuishi kwa niaba yao. Wananchi tunaiba na tukipata madaraka tunaiba zaidi, Iwe CCM au chama kingine chochote, vyote viko mikononi mwa watanzania wenzetu wenye hulka hizihizi. Kwa mtazamo wangu, ukombozi tunaohitaji sasa ni kifkra zaidi kuliko ukombozi wa kisiasa. Expectations kubwa sana juu ya vyama mbadala wa CCM ni janga lingine lijalo......as nothing will change much!
mwananchi wa Tanganyika!