Mkuu kakakiiza, Tatizo la Zanzibar, bado nitaendelea kudhani kuwa ni siasa. Kila upande wa muungano tangu kuundwa kwake, unakubalina kuwa Muungano una changamoto. Kwa miaka yote ya Muungano, hakuna jitihada za dhati zilizochukuliwa katika kutatua matatizo hayo. Hali hii inapelekea watu kuchoka kuendelea kuelezwa hadithi na matumaini yasiyo tekelezeka. kwa ujumla CCM imedharau sana maoni ya wananchi kuhusu kero za muungano. Matokeo ya dharau hii ya CCM, imejenga watu kuchoka. Sasa mwisho wa watu kuvumilia unapofika, hayo hujitokeza.
Hata kama kuvunjika kwa muungano kutaleta matatizo zaidi kwa wazanzibari, wao wanaona iwe iwavyo.