Kama kuna kitu mnajidanganya Wazanzibar basi ni hiki hapa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama kuna kitu mnajidanganya Wazanzibar basi ni hiki hapa...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KakaKiiza, May 28, 2012.

 1. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Katika mfulurizo wa ghasia zinazotokea Zanzibar na kusababisha uharibifu wa mali nimoja ya tatizo linaloitia doa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla hasa ukiangalia kwamakini unakuja kugundua siyo vurugu za kisiasa bali ni zakidini kwa mgongo wa siasa!!
  Lakini hawandugu zetu wazanzibar wanajidanganya padogo sana kwakudhani kufanya hivyo nikumaliza tatizo!!
  Nawalio wengi wanaojiingiza katika vurugu hizi wengi wao uelewa wao ni mdogo kwani wale wote wenye uelewa hawajiingizi katika huu upuuzi!!Nawalio wengi wanajidanganya kuwa zanzibar ikijitenga itakuwa kama DUBAI kitu ambacho siyo nawengine wanathubutu kusema lazima zanzibar iwe nchi yenye kufuata misingi ya sharia nasema ni uelewa mdogo wa wazanzibar wanaoleta vurugu tunaomba serikali iwadhibiti na ilitazame kwa jicho latatu!
   
 2. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu kakakiiza, Tatizo la Zanzibar, bado nitaendelea kudhani kuwa ni siasa. Kila upande wa muungano tangu kuundwa kwake, unakubalina kuwa Muungano una changamoto. Kwa miaka yote ya Muungano, hakuna jitihada za dhati zilizochukuliwa katika kutatua matatizo hayo. Hali hii inapelekea watu kuchoka kuendelea kuelezwa hadithi na matumaini yasiyo tekelezeka. kwa ujumla CCM imedharau sana maoni ya wananchi kuhusu kero za muungano. Matokeo ya dharau hii ya CCM, imejenga watu kuchoka. Sasa mwisho wa watu kuvumilia unapofika, hayo hujitokeza.
  Hata kama kuvunjika kwa muungano kutaleta matatizo zaidi kwa wazanzibari, wao wanaona iwe iwavyo.
   
 3. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Mkuu sawa yote uliyoyasema ni haki lakini ukiangalia sana tatizo siyo muungano tatizo ni udini uliotawala kama unakumbuka kuchoma nyumba za ibada halikuanza leo!!Nalenyewe linahusika vipi katika muungano??Kuchoma mabaa linahusika vipi kwenye muungano mimi hapa naona ni dini iliyojikita kwa mgongo wa vuguvugu la demokrasia!!
   
Loading...