Jipange sawasawa!!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2010
Posts
11,902
Reaction score
9,323
Hapo mwanzo Mungu aliumba ulimwengu na wanyama wake. Kila mnyama alipewa
miaka ya kuishi 30. Kati ya wanyama walioumbwa walikuwa Punda, Mbwa na
binadamu. Mungu akawauliza wanyama hao Je! unadhani miaka hiyo thelathini
inakutosha? Kila mmoja akajibu hivi:

Punda: Mimi nikae nikitumikishwa miaka 30, niwe kihongo miaka yote hiyo?
Loh! kazi hiyo ni kubwa sana . Mimi nipunguzie iwe miaka 10 tu inanitosha
bwana.

Mungu: Sawa wewe utaishi miaka kumi tu.

Mbwa: Mimi nikae nikilala nje miaka thelathini! Kula majalalani, kubweka
usiku kucha. Naomba unipunguzie niishi miaka kumi tu inanitosha.
Nitajitahidi kwa kipindi hicho kulala nje, kubweka na kulinda usiku kucha.
Watanitumia wapendavyo kunusa madawa ya kulevya, kukamata wanyama nk.

Mungu: Sawa, umri wako utakuwa miaka kumi.

Binadamu: Ha! Miaka 30 tu, nita enjoy nini mimi? Niongezee bwana.

Mungu: Sawa, niliyoipunguza kwa punda na mbwa utaongezewa wewe. Nawe
utaishi miaka sabini (30 + 20 + 20 = 70). Kipindi chako cha miaka 30
utaishi maisha yafaayo binadamu, miaka ishirini inayoongezeka utakuwa na
maisha ya punda, na miaka ishirini inayoongezeka utakuwa na maisha kama ya
mbwa.

Binadamu: Ahsante sana bwana na iwe kama ulivyosema.


Miaka 0 – 30+: Maisha mazuri sana (hayo ndiyo maisha ya binadamu). Maishaya kutafuta marafiki, maisha ya kulishwa, maisha ya kuwaandikia barua girl friends na boy friends hata wale ambao wanakupotosha wewe huyaoni hayo, kutafuta pen pal. Maisha ya kuangalia mtindo mzuri
wa nguo, nywele, kutembea kwa mikogo, kutuma message kila dakika,
kupigiana simu kila saa, ugomvi usio na kichwa wala miguu, kukasirika kwa mambo yasio na mbele wala nyuma, kujifunza
kuvuta bangi, kunywa pombe, kuhudhuria madisco n.k.

Miaka 35 – 50: (Maisha ya punda). Wengi wanajitegemea wameoa au kuolewa. Maisha magumu, unapanga chumba lakini mhh kodi sasa watoto watano na mke chumba kimoja, kibarua wa kubeba zege, kimbiza shilingi, huna muda wa kwenda disco tena au kuangalia mitindo mipya, hakuna kulala hapa. Watoto wanasumbua shule, wanaumwa, kadi nyingi za harusi, madeni hadi unawakimbia marafiki zako. Hii itaendelea hadi upite umri wa miaka hamsini.

50+ tuseme 60: Ms
taafu. Unakaa nyumbani, unalinda boma (maisha ya mbwa),
nyumba imebomoka huna pesa ya kurepair, nyumba inavuja, watoto wote
wameondoka wanahangaikia maisha yao na wake/waume zao. Huna jinsi wewe ni
kama mlinzi wa eneo ulilochagua.

Je! Katika maisha haya upo kundi gani? Jiandae hatua unayoendea ni ngumu
zaidi. Jipange, wakati ni huu.


JIPANGE SAWASAWA!!


Thought for today: I have found the paradox that if I love until it hurts, then there is no more hurt, but only more love.
-Mother Teresa
 
Nipo hapo kwa punda.!hongea na sir god ili nirud kule mwanzo
 
Hadithi yako hii Inanipa Kuamini ya kwamba Vitabu Vitakatifu (Bible &Quran), Chimbuko lake au Viliandikwa Kwa Kuzingatia mazingira ya Wazungu zaidi: Mfano; Neno Utupe Leo Mkate wetu wa Kila Siku na Sio Ugali au wali wa Kila siku; Hapa ni Kama 90% ya Wazungu Mlo wao ni mikate , burger na aina kama hizo.

Sasa Nikija Kwa hili la Wanyama akiwemo Mwanadamu Kupewa Miaka ya kuishi; Hadithi yako ni kweli kwa 100% ina hold water Kwa Wazungu, lakini Sio Kwa Wabongo; Unaona hapa Bongo ndo Kwanza kwenye Umri huo vizee vinateuliwa Kuwa viwakilishi vya Waganga wa jadi kwenye Katiba ya nchi.

Kwenye umri huo ndio tunaona Wagombea urais wengi wakijitokeza toka CCM. Wa-Bongo Tunaamini kwenye Uzee na ndio Maana tumeaminishwa na wazee ya kwamba vijana ni Taifa la kesho, slogan zinazofifisha harakati za vijana ktk Kuamua mstakabali wa taifa lao.

Kwenye Miaka 50+ ndio Miaka ya kutajirika na Kupiga Madeal kwa Wabongo; Hii ndio Miaka ya uporaji wa Mali za Umma na Washirika wako wa karibu.Hii ndio Miaka ya kujenga Mahekalu na Kuenjoy maisha.

Hadithi yako Ni ya kweli kwa WazunguLakini Haiwezi Kuwa applicable hapa Bongo.
 
Hapo umenena kabisa maana ndo maisha yalivyo
 
Hili kundi la katikati ndilo linaloninyanyasa mda huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…