Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,741
- 25,681
Katika maisha yangu nimekutana na wanachuo wengi, wengi wao waliniambia changamoto nyingi wanazokutana nazo vyuoni. Wengi waliingia vyuoni wakiwa watakatifu, watulivu lakini walipoondoka waliondoka wakiwa wengine kabisa.
Ninayakumbuka yote. Nimezungumza nao kwa mara nyingine tena na kuwauliza kuhusu kusimulia maisha yao hapa, wote wamekubali lakini nitatakiwa kutumia majina yao mengine kabisa.
Lengo ni nini? Kuna wanafunzi wengi wanajiunga na vyuo, naamini kwamba kupitia maisha ya watu hawa wanaweza kujifunza mambo mengi na kuwa waangalifu sana.
Ninaiandika kwa mtindo wa simulizi ili isikuchoshe, ili usiboeke, kwa hiyo utakaposoma, itaonekana kama ni simulizi lakini jua kwamba unasoma kitu cha kweli kabisa.
Nitakuelezea maisha ya wanafunzi watatu ambao maisha yao yalibadilika na kuwa machafu baada ya kuingia chuoni. Ungana nami ili uende kujifunza mengi.
Kwa kuwa humu kuna simulizi mbili zinaendelea na Instagram ipo moja, hii nitaihamishia huko japokuwa utatakiwa kusoma angalau kidogo upate picha ya kile kitakachoendelea.
Kwa wale ambao hawana akaunti Instagram, wasijali, bado simulizi nyingi zitakuja humu hivyo hawatakiwi kuogopa hata kidogo. Kwa wale wa Instagram, tukutane huko. Huu ni mwanzo wa mambo haya yanayotokea chuoni ambayo inawezekana kabisa wengine wakawa hawayajui ila kwa sababu nilisimuliwa, sina budi kuwahadithia.
***
NAJMA SALUM:
Kwa jina aliitwa Najma Salumu ambaye baada ya kuingia chuoni alipewa jina la Naj ambalo baadaye akalizoea na kulitumia mpaka sasa.
Katika kipindi alichokuwa akiingia chuoni, alikuwa na miaka ishirini na mbili. Alikuwa msichana mrembo mno, macho ya goroli, lipsi nene huku katikati ya meno yake akiwa na mwanya uliompendezesha kila alipokuwa akikenua au kucheka.
Siku ya kwanza alipoingia chuoni na kuhudhuria kipindi darasani, wanaume walichanganyikiwa. Alikuwa msichana mrembo mno, alivalia suruali ya jinsi, fulana huku kwa nje akiwa na baibui jeusi na ushungi kichwani mwake.
Wanaume walimtolea macho, uzuri wake ulionekana dhahiri. Kila mwanaume aliyemuona akatamani kuwa naye kwa kuwa tu alimvutia kila mtu. Naj alikuwa mpole wa sura, muda mwingi alikuwa kimya, hakutaka mazoea na wanaume kwa kuwa aliwajua vilivyo walivyokuwa walaghai.
Wengi wakatamani kupata namba yake ya simu, wamuone katika WhatsApp ameweka picha gani, lakini ukiachana na hayo, pia walipenda kuona akaunti zake za Instagram na Facebook alikuwa na picha gani kwani kumuona yeye mwenyewe haikuwa ikitosha bali walihitaji kuona na picha zake nyingi, chumba chake kilikuwaje na hata kama ana ndugu, je, walikuwa wazuri kama alivyokuwa?
Wanaume wakaanza mazoea, kila mtu aliyesimama mbele yake alijifanya mcheshi ili kuweza kumtega msichana huyo. Naj hakutaka kubaki kimya kwa kuwa aliamini kwamba hao ndiyo ambao wangemsaidia kwenye masomo yake hivyo akaanza kuwazoea, walipohitaji namba ya simu, bila kinyongo akawapatia.
Hakuwa na simu ya smartphone, alikuwa na zile zinazoitwa Nokia ya Torch kwa maana hiyo hakuwa na ‘access’ ya kuingia Instagram au Facebook kwa kutumia simu yake.
“Unatumia simu hii?” aliuliza mwanaume mmoja huku akionekana kushangaa.
“Ndiyo! Kwani kuna ubaya?”
“Hakuna ubaya! Sasa utaingia vipi Instagram na Facebook?” aliuliza mwanaume huyo, hiyo yote ilikuwa ni kutaka kujua kama binti huyo alikuwa na akaunti huko.
“Mbona kawaida. Cha msingi mawasiliano!”
“Kwa hiyo Instagram haupo?”
“Yeah!”
“Hata Facebook?”
“Huko ndipo sipapendi kabisa.”
“Ooppss! Jamaniiiiiii!”
Huyo alikuwa Ismail Shabani, mwanaume aliyekuwa na mwili mkubwa, kifua kipana na alinyoa ndevu zake kwa mtindo wa O. Kichwani alikuwa na afro fulani hivi ambalo alilipaka mafuta na kung’aa kupita kawaida.
Alitembea kwa mbwembwe, alidunda kiasi kwamba wanawake wengi wakaupenda mwendo wake. Aliamini kwamba kwa kuanza kuongea na Naj basi angefanikiwa kile alichokuwa akikitaka.
Wakaanza mawasiliano kwenye simu. Kwa maelezo ya Naj, anasema kwamba Ismail alijua kuzungumza na mwanamke, alijua mwanamke alikuwa akihitaji nini na kwa wakati upi.
Sauti yake kwenye simu ilikuwa ikibadilika, ilikuwa nzuri flani hivi, Kiingereza alichokuwa akiongea ni kama kile cha Wamarekani ambacho kilimchanganya sana Naj na kuhisi kwamba mwanaume huyo angekuwa sahihi katika maisha yake.
Japokuwa kulikuwa na wanaume wengine waliokuwa wakimfuatilia lakini akajikuta akiwa karibu zaidi na Ismail ambaye alikuwa hashikiki, kila alipokuwa akiamka, alikutana na meseji, darasani, meseji, yaani mpaka ikawa kero.
“Shigongo! Nyie wanaume mkihitaji kitu mnasumbua sana. Huyu Ismail alikuwa akinisumbua mpaka ikawa kero, yaani alikuwa akinipigia simu mara kwa mara hata zaidi ya wazazi wangu waliokuwa wakinisomesha kabla ya kufika hapo,” aliniambia Najma.
“Ikawaje baada ya hapo?” nilimuuliza huku nikiwa na hamu ya kufahamu kilichokuwa kimetokea kwani kila alipokuwa akiniambia hivyo, kulikuwa na hadithi fulani iliyokuwa ikinijia kichwani, sasa nilihitaji yeye aikamilishe.
Najma anaendelea kusimulia kwamba siku moja alikuwa darasani akijisomea. Wakati akiwa kwenye utulivu mkubwa huku wanaume wakiwa pembeni wakimwangalia kwa matamanio, Ismail akafika mahali hapo huku akiwa na kiboksi fulani ambacho mara ya kwanza Naj hakujua kulikuwa na nini ndani.
Alipofika, akakiweka juu, akatoa tabasamu na kumwangalia macho yaliyoeleza hisia kali za kimapenzi. Kabla ya kuzungumza kitu, Ismail akatoa tabasamu pana.
“Vipi Naj!” alimsalimia.
“Safi! Karibu!”
“Nashukuru!”
Akanyamaza, wawili hao wakabaki wakiangaliana tu. Hakukuwa na mtu aliyeongea kitu chochote kama kwa muda wa dakika moja hivi.
“Nimekuletea zawadi,” alisema Ismail huku akimkabidhi kile kiboksi.
“Zawadi gani?”
“Wewe fungua tu!” alisema na hivyo Naj kuanza kufungua, japokuwa hakujua kuhusu ndani lakini alijua kabisa kwamba hiyo ilikuwa simu aina ya Nokia kwani nje ya boksi lile iliwekwa picha yake. Alipofungua, kweli akakutana na simu.
“Nimekuletea simu! Nataka tuwasiliane kwa WhatsApp. Nakumiss sana kule jamani, ikiwezekana uwe na akaunti ya Instagram rafiki yangu,” alisema Ismali huku akiachia tabasamu. Uso wa Naj ukabadilika kidogo, akaonekana kama ana hasira fulani hivi.
Unajua nini kiliendelea kuhusu huyu Naj? Na kwa nini alikuja ofisini kwangu na kunielezea hayo yote?