Jehanamu ni nini?

nebuchadnezzer

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2013
Posts
246
Reaction score
344
View attachment 45647

Jehanamu au Jehanum ni Neno lenye chimbuko la kiyunani Gehenna, ambalo limetafsiriwa kutoka katika lugha ya kiyahudi ge-hinnom Ikiwa na maana bonde la mwana wa Hinomu.. Hili ni eneo lililokuwa kusini mwa mji wa Yerusalemu, lililojulikana kama Tofethi ambao watu wasiokuwa wanamcha Bwana walikuwa wanalitumia kuwatolea watoto wao kafara kwa kuwapitisha motoni kwa miungu waliyoikuta huko Kaanani. Jambo ambalo lilikuwa ni chukizo kubwa sana kwa Mungu, ambalo nalo pia lilikuwa ni mojawapo ya mambo yaliyowafanya wachukuliwe utumwani Babeli.

JEHANUM NDANI YA BIBLIA
Lakini baadaye tunaona Mfalme Yosia alikuja kulinajisi eneo hilo , likawa halitumiki tena kufanya mambo yao ya kichawi,
2Wafalme 23:10 “Naye akainajisi Tofethi, iliyomo katika bonde la wana wa Hinomu, ili mtu asipitishe mwana wake au binti yake motoni kwa Moleki.”
likabakia kutumika kama dampo la jiji, na bonde la kutupia miili ya watu waovu, pamoja na wanyawa waliokufa pamoja na kuchoma takataka na kila aina ya uchafu wote uliotoka mjini..Na hiyo ilipelekea bonde hilo kuwa la kinyaa sana na wakati wote kuwa linawaka moto, na moshi mkubwa unaopanda juu pamoja na harufu kali sana, kutokana na kwamba kila wakati uchafu ulikuwa unaingia..

FUNZA WA JEHANAMU
Sasa zile sehemu ambazo moto ulikuwa haufiki vizuri, kulikuwa na funza wengi sana, ambao walipita katikati ya mizoga ile iliyokuwa imetupwa, ni eneo ambalo hakuna mtu angeweza kukaa hata dakika mbili au kusogea karibu na ukawa sawa. Kama ulishawahi kuona jalala kuu la manispaa au jiji basi fahamu kuwa huo ni mfano mdogo sana ukilinganisha na GEHENA ilivyokuwa..bonde hilo lilikuwa linatisha sana. Funza wa jehanamu walikuwa ni wagumu kufa kwasababu walikuwa ni tofauti na funza wengine.

Na ndio maana Bwana YESU alitumia mfano huo, kueleza picha halisi ya kuzimu ilivyo kwa wale ambao watakufa katika dhambi zao. Alisema..

Ni wazi kuwa hakuna mtu anayependa kuwepo sehemu yeyote chafu, basi hiyo inatupa chachu pia tujiepusha na kuzimu kwasababu kuzimu ipo kweli na si mahali pazuri hata kidogo huko hakuna raha, ukishajikuta kule, utakuwa katika mateso siku zote ukisubiria hukumu ya siku za mwisho kabla ya kutupwa katika lile ziwa la moto..

JE UPO NJE YA KRISTO AU NDANI YA KRISTO?
Kama upo nje ya Kristo, wakati ndio huu, tubu sasa, mpe Bwana maisha yako naye atakupokea..Na kukusamehe kabisa, kwasababu mbingu amekuandalia wewe, hivyo daima hataki nafasi yako ipotee.

Ubarikiwe.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…