Je, wamefikia malengo?

Ngisibara

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2009
Posts
3,413
Reaction score
2,276
Kuna wanasiasa ambao walikuwa mabingwa wa kutetea chama na viongozi wao hapa JF kwa masaa 24/7, yaani hata uanzishe thread ya kukosoa CCM saa 7 usiku baada ya dakika tatu utaona umejibiwa.

Leo najiuliza na kutafakari au ndio yale maneno ya mama kuwa kuna wakuja na ndio hao hao wana vinongwa nongwa?

Kwanini hawaji JF kutetea mazagazaga kama zamani, Wapi Hussein Bashe, Juliana Shonza, Nape Nnauye, Mwigulu Nchemba, Amos Makalla , January Makamba au mkipanda V8 JF haipatikaniki?

Tumewamiss sana angalau mapumziko ya kimasimasi yajayo njoni muhibiri sera zenu e. g hamuoni kama itakuwa faida 2025 kama mtaingiza Tozo mbalimbali kwenye wizara zenu?
 
NAWE, Nawe huoni kuwa walichumia juani Sasa wanalia kivulini? Unataka waje Tena kujianika juani na joto lote hili?
 
NAWE, Nawe huoni kuwa walichumia juani Sasa wanalia kivulini? Unataka waje Tena kujianika juani na joto lote hili?
Kibuyu cha asali ndio kwanza kimefunguliwa wapo kidole cha tatu? kweli hawawezi kuja huku.... Basi angalau wamkaribishe na mwenzao Pascal Mayalla
 
Kibuyu cha asali ndio kwanza kimefunguliwa wapo kidole cha tatu? kweli hawawezi kuja huku.... Basi angalau wamkaribishe na mwenzao Pascal Mayalla
Yule kikwao maana yake njaa kali, kwani Hawajui, asije kula kwa kutumia mikono yote ikawa aibu kwa iliyemfungulia mlango. πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…