Je, Tundu Lissu kumstaafisha Siasa Abdulrahman Kinana?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
118,945
221,396
Kwa Taarifa nilizonazo ni kwamba, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu anapanga kufafanua na kupangua Upotoshaji wa Mzee Kinana, huu alioutoa leo kwa Waandishi wa Habari.

Hatuna haja ya kuyarudia tena aliyoongea Mzee Zaidi Kinana, maana ni dhahiri kila mmoja amemsikia, bali bila hata akili kubwa sana utagundua kwamba uwezo wa Mzee Kinana umekwisha, hana tena ule weledi aliosifiwa nao awali, nadhani ni kwa sababu ya Uzee (Kila lenye mwanzo lina mwisho, huwezi kuwa na zaidi ya miaka 80 ukawa na akili zilezile za ujana)

Swali letu ni hili, Je Spana za Lissu Zitamstaafisha Rasmi Siasa Mzee Kinana ?
 
Leo ndio nimeamini CCM siyo ile yenye majigambo! Niliamini watakuja na jibu lenye hoja! Kumbe CCM hoi imezeeka, haina uwezo tena, sasa ni kuipumzisha tu. KTK majibu ya Kinana, alishindwa hata kutamka jina Tanganyika!
 
Mi nijibu Kichwa cha Mada tu:
Huyo mtu si alishastaafu chini ya Magufuli?
Hawa huwa hawastaafu, mtu wao akiingia madarakani wanarudi haraka kuinyonga nchi

Huyo mtu kazi yake maalum ndani ya CCM ni kuhakikisha CCM inaendelea kuwa madarakani kwa njia yoyote ile. Huyo na Januari ndio walikuwa 'architects' wa wizi wa kuru kwa kutumia mtandao.

Ni wakati sasa huyu mtu afuatiliwe kwa karibu zaidi, kwani ana uchafuzi mwingi sana huyu..
 
Swali letu ni hili, Je Spana za Lissu Zitamstaafisha Rasmi Siasa Mzee Kinana
Ngoja nirudi. Sasa nimesoma mstari wa mwisho wa mada, na jibu ni HAPANA.
Huyo hawezi kustaafu chini ya utawala wa viongozi wanaomtegemea katika kufikiri. Samia atafanya nini bila ya kuwepo Kinana? Huyo ndiye 'Mastermind', 'Think tank' wa chama chote kwa sasa hivi.
Hata angependa kustaafu, hawatamruhusu, hasa wakati huu hali inapoelekea kuwa ngumu sana kwa chama hicho.
 

..tatizo sio umri wa Mzee Kanali Kinana.

..kilichomponza Kinana ni kutetea uongo.

..kinachompandisha chati Lissu ni kusimama upande wa ukweli, na haki.
 
Tena vibaya mno, kinana kwisheni
 
Yaani mpaka msahau katiba mpya, akijibu tunarudi tena, safari hii Nchimbi akiwa Mwanza atavurumisha maroketi
 
Ngoja tuone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…