Niko na mwanangu wa siku nyingi tunajadili hoja mtambuka.
Leo tunajadili hoja mtambuka inayohisi uwepo wa Mungu.Swali ni je Mungu Yupo?.Namtazama kwanza kwa makini kisha namuuliza kwa nini unafikiri kuhusu suala hili lina umuhimu gani?Kwa kuwa mimi naelewa kwamba Mungu yupo namwambia tu ndio yupo?Kwa hakika kabisa ananitaka nithibitishe iwapo Mungu yupo.Namatazama kwa makini na kumwambia je wewe unaweza kuthibitisha iwapo wewe upo?
Kwa hakika anajaribu kujenga hoja tofauti:
Hoja yake ya kwanza ni kwamba yeye yupo kwa sbb ninamuona,namsikia na kumgusa.Yaani ananipa uthibitisho kwa misingi ya "sensory perception"nami kwa wepesi namwambia je ukiwa katika usingizi mzito unasikia,akajibu hapana,je unaona au ukiguswa unasikia?anajibu hapana.Namaliza kwa kumuuliza je Kwa kuwa unapolala zile sensory perception zinakuwa chini je ina maana kwamba kwa wakati huu basi watu wengine hawapo?Anashtuka kidogo lakini kwa ajili ya kumsaidia asichoke na mwambia kuwa uwepo wa Mungu si relative na kwamba ukitaka kuulewa uwepo wako ni lazima kwanza uweze kuuelewa uwepo wako wewe mwenyewe na jambao la muhimu ni kujua kuwa dini si ushahidi wa uwepo wa Mungu na kwamba hizo ni jitihada tu za kutafuta ukaribu naye ukaribu ambao kama binadamu tuna uhitaji sana.Na hata wale ambao hawaamini katika uwepo wa Mungu kwa maneno yao huwa wanamtafuta Mungu sana na kutaka kuwa nae karibu
Je.wewe unafikiri nini kuhusu uwepo wa Mungu