binti huyu ameajiriwa kuuza duka la dada mmoja jirani na ofisini kwangu,
anaonekana anajiheshimu na anaonekana mcha mungu,
mimi binafsi nlishatendwa na niliyekuwa naye hivyo nimechoka na haya maisha ya kuwa mpweke nahitaji kuoa,
baada ya kumchunguza binti huyu kwa miezi kadhaa nmetokea kuridhika nae,
hivi sasa tuna mwezi mmoja tangu tuanze mahusiano.
Nikiwa najiandaa kwenda kwao nliamua kumuuliza kuhusu wazazi wake na maisha ya kwao kwa ujumla,
binti huyu akiwa ktk hali ya huzuni alianza kunisimulia historia yake kwa ufupi,
ni mtoto wa nne ktk familia ya watoto watano,mamake alifariki na kumuacha mdogo
babake alikuwa anafanya kazi kwa wahindi na sasa kazeeka hana kitu,
binti huyu amemaliza frm 4 na alijisomesha mwenyewe kwani familia ilisambaratika baadhi hawajulikani waliko,
akiwa masomoni aliwahi kukatisha masomo na kufanya kaz za ndani sehemu tofauti na aliwahi kubakwa na mwajiri wake,
pia alifikia kujiuza ili apate pesa ya ada,
aliwahi kubakwa na askari usiku,
alifanikiwa kumaliza frm 4 na kupata cheti.