As salaam.
Ndugu zangu watanzania Jana nimejikuta nawakumbuka sana kwa utu na wema wenu haswa kwa wale baba au mama wenye nyumba zao mjini tunazopanga sisi ambao tunaanzaga maisha na kutengana na family zetu.
Katika hali ya kuongeza shule niliona nibadilishe madensa ya bongo nikajirusha nchi za wenzetu huku bara la asia, Nimepanga mtaani nyumba ambayo naishi na baba mwenye nyumba yeye anaishi floor ya chini na sisi wapangaji tupo floor za juu na mtu mweusi nipo peke yangu na nimekuwa nikilipa kwa wakati kodi yangu ya mwez ila mwezi huu mambo hayakuwa mazuri kutokana na pesa kuchelewa kuingizwa na ilikuwa ni kama Siku moja imepita, Cha kushangaza narudi home mida ya saa3 hivi usiku nakuta kufuri mlangoni kwangu sababu wao huwa wanaweka komeo na kitasa vyote kwa pamoja na unaweza funga vyote. Kiukweli mie sikuwa naelewa maana ya kuweka huu mfumo ila tangu jana nimeelewa maana ya kitasa na komeo.
Kuna mambo mengi sana nimeyakuta huku ila nilichukulia kawaida sana, mfano mzur ni swala la kujichanganya yaani ni wabaguzi hatari, Pili hata darasan utakuwa automatic wausi upande wao na wa Asia upande wao. Ila hili la jana nilijikuta naongea hadi kiswahili mbele ya umati uliokuwa unashuhudia lile ligi yaani nilitukana kila aina ya tusi haswa pale nilipokumbuka wanavyoishi huko kwetu kwa raha na kiburi, Hahahaa hakika huyu mzee alikuwa ananiona sina mda nao ananidharau mapigo yangu ila sasa naamini kanielewa vizuri.
Hapa nipo nawaza cha kufanya nataka niendelee kuchukua taiz zaidi kama ya Jana maana hadi kipindi cha mwisho mimi ndo nilikuwa mshindi wa magoli ya kutumbukiza na zaidi nimegundua ni muoga hatari maana hadi sasa akiniona anaingia ndani na pesa ya kodi kasema nimpelekee dalali alienipangisha. Hii ni baada ya police kumweleza kama nikienda mahakamani naweza mshinda na hata kumfunga kutokana na sheria yao juu yetu Maana alikuwa na deposit yangu zaidi zaid ya laki6 ambayo ndo mdhamana wangu kwake.( Hii inarudi naporudisha nyumba au kufidia naposhindwa kulipa baada ya mwezi au kuharibu chochote)
Binti yake vasha leo hajanisalimia kabisa nimeumia sana maana ndo mtu pekee alikuwa anajua lugha ya malikia na mtoto nilikuwa namkubali sana maana hata ile sauti yake nitaikosa jamani au kuja kuona navyopika Swahili food. Tafadhari ndugu zangu nipeni mawazo nini nifanye ili vasha aendee kuniuliza South Afrika ipo vipi maana wao ukiwambia Tanzania hawaelewi wanaijua tu Afrika nzima ni South Afrika.
NOTE: Roho nyeusi haipo kwa mtu mweusi pekee hata hawa tunaowabudi kuwa na roho nzuri si kweli wana roho nyeusi hata zaidi yetu sisi. Kwa sasa nawachukia wahindi wote isipokuwa vasha pekee. Eeh Mungu nisaidie nirudi salama Tz nisije ishia gereza la kihindi Maana hapa najiandaa kwenda kununua panga.