JamiiForums Vacancy: Intern (4)

Kwny Pannel ya interviewee pawepo na watu kama Pascal, Maxen , hahaha hz ajira tutaziskia tu
Hapana, hatutaki ID ya mtu. Kuna maswali utaulizwa yataeleza kama wewe umekaa muda uliosema au unazingua tu
 
Kiizungu hapo kwangu ndio shida kubwa ila sifa zote ninazo
 
Hapana, hatutaki ID ya mtu. Kuna maswali utaulizwa yataeleza kama wewe umekaa muda uliosema au unazingua tu

Nitakapoulizwa nani aliendika thread ya kwanza ya Mh. Kitwanga kujibu swali bungeni akiwa amelewa nikashindwa kujibu nitakua nishazingua. Hayo maswali bila ID yatazingatia pia watu ambao hawapo active kila siku kiasi vitu vingi vinawapita?
 
nimeona kigezo kimoja muombaji awe na ID yenye muda usiopungua mwaka mmoja na iliyokuwa hai, kwahiyo kuna haja ya kutaja ID yako ndani ya hiyo cover letter?

kama sivyo watawezaje kujua muda wa ID ya muombaji!!
kama utapita kwenye first selection nahisi ndipo itakapohitajika hiyo ID ya jf ukiwa nao kwenye proceeding interviews.
 
na cover letter ya intern eti una mention post?
 
Naomba kuuuliza kuhusu post 4 zilizotangazwa na JF "INTERNS" . Naomba kufahamishwa machache kabla sijafanya uamuzi mgumu;
1. Mosi, Naomba kujua kama ni "Paid" maana kwa kawaida ama sehem nyingi Interns ni kazi za kujitolea na kujifunza zaidi ambapo interns mwenyewe anajigaramia ili apate ujuzi ama uzoefu kabla ya kuingia ajirani rasmi.

2. Napeda kufaham kama baada ya muda fulani hawa 'Interns" watakuwa employed ama promoted to permanent positions as per area of their interest/ specialization ama after a time watalazimika kwenda kutafta ajira sehem nyingine baada ya kumaliza internship yao JF?

Naomba kuwasilisha.
 

Sasa mbona Swali lako uliloliuliza tayari umeshajijibu mwenyewe hapo katika Kipengele chako cha # 1 Mkuu? Na kuhusu Kipengele chako cha # 2 nadhani hapo Jibu sahihi ni Majaliwa yake tu Mwenyezi Mungu pekee. Mwisho kabisa nakushauri jibiidishe vyema katika Kulielewa neno hilo la INTERN ( INTERNS ) tafadhali kwani nadhani kama ungekuwa umelielewa vyema kabisa wala usingekuja na haya Maswali yako Mawili uliyoyawasilisha hapa Mtandaoni.
 
Na kingine Cha kuongezea hapa.
Anasema anahitaji majibu kabla hajachukua maamuzi magumu,maamuzi gani magumu hayo?kutuma CV kwa email ndio maamuzi magumu?Watoto wa siku hizi ni wavivu mno wa kujishughulisha na pia hata kufikiri ni wavivu mno.
Mimi ningemuona mjanja angeomba akasubiri kufanya interview then akishapata hyo nafasi haya maswali yake ndio angeenda kuulizia kule kule kwenye kazi na akiona hailipi anaweza kuacha tu hakuna mtu atamlazimisha.
 
Kwakua una cheti changu cha kuzaliwa ndio maana unathubutu kunijumuisha 'mimi' na watoto, sijui wanao?
Nadhani ni suala la uelewa tu, wengi wenu naona mmesoma thread yangu ili mnijibu. Na majibu unaweza kutoa yeyote hale hata kama yanatoka nje ya mstari, badala ya kusoma muelewe then ndio mjibu, tena sio kuinijibu mimi binafsi ila kwa faida ya wengine wengi wanaotatizika hapa.

Pili, Nafasi zipo 9 lakini hata kama unafit nafasi zote, lakini masharti ni kuomba nafasi moja pekee. Hapa ndiyo hasa maamuzi magumu niliyomaanisha. Hata hivo nakushukuru kwa kushiriki kwenye mjadala.
 
Sasa Kama unafit kwenye nafasi zote kwa nini uombe nafasi ya internship?
Nafasi za internship ni kwa ajili ya watu wasio na uzoefu lengo ikiwa ni kujifunza kazi.
Sasa kumbe wewe una vigezo vya kuomba kazi zingine halaf unataka kuziba nafas za vijana waliotoka chuo.
Ndio maana Kuna mchangiaji mmoja alisema inawezekana hujui maana ya internship.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…