Nitangulize shukrani zangu za dhati kwa ushauri wenu ambao unasaidia wengi humu!
Nina mwanangu wa kiume ambaye ana miezi 9 sasa ameanza kutembea,
tatizo la huyu mtoto ni kuwa hataki chakula cha aina yoyote ile!iwe uji,ugali,ndizi,viazi,maziwa,juisi,
yani kidogo ukimpa chungwa ndo atakula angalau kipande tu + kunyonya basi.
Nimehangaika hospitali lakini tatizo hili halijakoma na mda mwingine analia kwelikweli mpaka nachanganyikiwa
hospitali wamenipa MULTI-VITAMIN SYRUP
yenye VitaminA,D3,B1,B2,B6,B12,C,Niacinamide,D-Panthenol
nimempa lakini hamna kitu,naomba msaada wenu jamani!njia gani ya ziada naweza kusaidia huyu mtoto
MziziMkavu na madaktari wenzio wote humu