J a n i

simba29

Senior Member
Joined
Jun 22, 2011
Posts
193
Reaction score
67
Katika maisha yangu, nimekuwa taabani ,
Kwenye huu mti wangu, ukiwapo mashakani,
Kila penye jua chungu, hujikalia pembeni,
Ni maisha yangu jani, katu hutoyatamani,

Kwangu sithaminiki, nafuu haipatiki,
Popote sitakiki, uchafu sihitajiki,
Nachomwa kimshikaki, mazingirani mikiki,
Ni maisha yangu jani , katu hayatamaniki,

Mti wangu naulisha, kujishibia maisha ,
Na chakula chakutosha, kwa juhudi nazalisha,
Mti nikinufaisha, haraka hunidondosha,
Ni maisha yangu jani, katu hayatamaniki,

Wanyama nawalisha, wengine kusjibika,
Na wagonjwa natibisha, afya njema kuimarika,
Kivuli hushamirisha, kwa amani hustareheka,
Ni maisha yangu jani, katu hayatamaniki,

Maisha yangu ni duni, mti wangu haunijali,
Hali yangu taabani, usiku kucha silali,
Maumivu ya moyoni, mti wangu upo mbali,
Ni maisha yangu jani, katu hutoyatamani.

0655880157

?2015
 
dotto C Chamchua njoo uone mambo huku.
naona wiki mbili hizi washairi wamechamka Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…