To me, solution rahisi ya mgogoro huu ni kuundwa kwa mataifa matatu, jirani, yatakayoishi kwa amani;
1. Taifa la Jordan.
Ukizingatia kuwa zaidi ya 50% ya wananchi wa Jordan pia wanajitambulisha kuwa ni Wapalestina, akiwepo Malkia wa sasa wa Jordan, so hakuna ulazima wa kuanzisha taifa lingine la kipalestina bali kuunda taifa kubwa la Wapalestina kwa kuipanua Jordan ya sasa itakalounganisha pia eneo la West Bank, mji wake mkuu ukiendelea kuwa Amaan kama ilivyokuwa kabla ya 1967.
2. Taifa la Gaza/Palestina(jina lolote watakalolipenda) lenye makao makuu yake kwenye mji wa Gaza, au kuwe na taifa kubwa la Misri linalounganisha eneo la Gaza lenye makao makuu yake Cairo.
3. Taifa la Israel kwenye maeneo yaliyobaki, taifa hili litaunganisha Wayahudi na Waarabu wanaokaa kwenye maeneo hayo kwa sasa, hii itakubalika kwa sababu waarabu wengi kwenye maeneo haya wanapenda zaidi kuwa kwenye taifa la Israel kuliko kuwa Palestina.