Kama ni ATX natumai itakuwa ni motherboard ya muda kidogo. Na inawezekana kabisa kuwa kuna pahala umeset jumpers wewe mwenyewe, maana mobo mpya nyingi hazihitaji manual setting ya jumpers. Kama PC inawaka na kujizima ghafla, mara nyingi hiyo ni ishara ya setting za jumpers kuwa siyo sawa. Kama screen ina flash kabla ya kuzimika, ni ishara kuwa memory ziko okay, lakini kama screen haionekani kabisa, basi tatizo laweza kuwa katika memory iwapo vingine vyote viko sawa. Pia check kama kuna sehemu katika cables umegeuza, yaweza kuwa umechomeka jumpers pahala pasipo, au peripheral cables za cd drive or hdd zimegeuzwa. Kwa kumbumbukumbu zangu kwa ATX mobo, hilo tatizo laweza pia kutokana na ku-overclock au ku-underclock cpu kupita kiasi cha tolerable voltage.