Iraq inajengwa upya

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
18,433
Reaction score
26,993
Baghdad inaendelea kunawiri, sio ile Iraq ya mwaka 2003 tena. Miundombinu inarejea, miradi inaongezeka, na mwelekeo wa nchi umebadilika kuelekea maendeleo ya ndani.

Kwa upande wa Wakurdi, Erbil (moja ya jimbo la Iraq) nako kumejengwa kwa kasi. Kuna kauli kwamba kufikia mwaka 2027 hakutakuwa na barabara hata moja ya vumbi. Ni eneo lenye uwekezaji mkubwa na pia kuna kambi/uwepo mkubwa wa kijeshi wa Marekani.

Miaka miwili tayari imepita, na sasa Iraq ipo kwenye miradi mikubwa ya kuifanya iwe nchi ya kisasa, kuanzia barabara, nishati, huduma za miji hadi ajira.

Katika muktadha huu, Muqtada al-Sadr, kiongozi mashuhuri wa Kishia nchini Iraq, alikataa kuiunga mkono Iran katika harakati zake za kijeshi. Alisisitiza kuwa vipaumbele vya Iraq ni kuwapatia wananchi maisha bora, si kuyarudisha maisha ya vita. Ujumbe wake ulikuwa wazi, kwamba,

"Kujenga uchumi na ustawi wa Wairaq ndio kipaumbele cha kwanza."

Je, hali ikoje katika nchi zenu ambazo hazina vita, zinatumia amani hiyo kujenga maisha bora ya wananchi, au zinapoteza fursa hiyo?
 
Mkuu alobomoa nani? Nyinyi makafiri sindo mnasema waarabu hawana akili? Naomba nioneshe mji mmoja wa makafiri ukiacha ya South Afrika upo kama huo hapa Africa
 
Babel Huwa haikati tamaa
Ingawa haiwezi kudumu Kwa sababu ikipata nguvu TU inapata kiburi
 
Babel Huwa haikati tamaa
Ingawa haiwezi kudumu Kwa sababu ikipata nguvu TU inapata kiburi
Wanajenga maeneo hayo tu, pale ilipokuwepo Dola ya Nebukaneza hapajengeki sawa sawa na unabii wa Isaya

Sadam Hussein alijaribu kujenga akakwama na mwisho akaishia kunyongwa


Sasa hivi pale ni Magofu tu

Isaya 13:19–20
“Babeli, utukufu wa falme, fahari ya kiburi cha Wakaldayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora zilipoharibiwa na Mungu.
Hautakaliwa tena, wala hautakaa milele katika vizazi vyote.”

Yeremia 51:26
“Hawatatoa jiwe kwako liwe jiwe la msingi, wala jiwe la kona; bali utakuwa ukiwa milele.”

Yeremia 50:39–40
“Haitakaliwa tena kamwe; itakuwa ukiwa milele.”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…