Inakuwaje sometimes tunayakinisha UWONGO ?

Judgement

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2011
Posts
10,326
Reaction score
4,789
Iko misemo ukiisikia tu , akili haihitaji kufikiri kusudio lengwa .

Mathalan ukisikia :
> Utaula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua !
> Chelewa chelewa utakuta mwana si wako!
> Hasira za Mkizi , furaha ya Mvuvi .
Etcetera

Na napata shida kiakili kukubali semi kama :
> Akili ni nywele , kila mtu ana zake!
HAPA ni kuyakinisha uwongo .
Maprofesa kibao ndiyo wanamiliki viaraza (vipara) itakua hawana akili kwa ukosefunywele ?
> Aliye juu mngoje chini .
Hii pia uwongo , asiposhuka je?

Ushauri wangu , tutumie misemo inayoendana na ukweli .
Ama kuna mwenye pingamizi?
 
Kwengineko utakutana na
"Kuvuja kwa pakacha , nafuu ya mchukuzi"
Nafuu hapa inatoka wapi ?
Ilhali mchukuzi mali yake inavuja?
Kwanini isiwe ,
"Kuvuja kwa pakacha , hasara ya mchukuzi" ?
Aidha
"Mficha uchi hazai"
Ni uchi gani wa binadamu usiyofichwa ?
Ukikatiza mtaa wa Congo ukiwa uchi , ukapanda sokoni Kariakoo , ukashuka , kisha ukatobokezea Mnazimmoja saa 6 mchana!
Ndiyo utazaa sana?
 
"sauti ya kumtoa nyoka pangoni"
huwa najiuliza nyoka yupi? pango lipi?
kwanini isiwe sauti ya kumtoa chura dimbwini???
mi naona huu msemo wa uwongo sana
 
Jingine utasikia 'atakaye shindwa kulipa bill ya umeme atumie kibatari'
 
Jingine utasikia 'atakaye shindwa kulipa bill ya umeme atumie kibatari'

Nikisikia neno "umeme" unanikumbusha neno "Tanesco" na nikiikumba Tanesco napata kichefchef !
 
Nikisikia neno "umeme" unanikumbusha neno "Tanesco" na nikiikumba Tanesco napata kichefchef !
pole mkuu nami sikupenda bali ndio hicho kichefuchefu hivyo nikaona bora nitoe nje kisije nidhuru mwilini...Lol!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…