Tanzania tumeingia katika hatari kubwa ya kuchanganya mambo ya elimu kuendeshwa kisiasa....Hali imekuwa mbaya zaidi pale ambapo mpaka waziri wa wizara husika baadala ya kutumia weledi anajikita kisiasa zaidi bila tafiti yoyote.....
Leo hii ukiuliza jamii nini kipya katika elimu utaambiwa ELIMU BURE ila bila kupepesa macho ukiniuliza mpaka sasa waziri wa elimu kaleta nini kipya yeye kama yeye katika mpango kazi wake ili kuinua elimu ukweli hakuna.....
Elimu ya kujitegemea ni elimu ambayo watoto waliyokuwa wanapatiwa iweweze kujiendeleza wenyewe baada ya kumaliza elimu.....
Elimu hii huwezesha wanafunzi pindi wamalizapo elimu yao kuweza kujiajiri wenyewe.......
WAPI TUNAFELI???
Kwanza wizara husika haina mkakati wa dhati kabisa wa kuinua elimu hii yaani ipo kwenye makaratasi ila ufuatiliaji ni zero...
Pia uchanganyaji wa siasa na elimu yaani lei hii mwalimu hana mamlaka yakumwambia mtoto akalime kwani akimwambia mzazi atasema kwa mwenyekiti au diwani hivyo wanawalinda wapiga kura wao na si mwalimu.....
Pamoja na hayo baadhi ya walimu na walimu wakuu wamekuwa wa kifanya hii(EK) kama miradi yao binafsi pasi na kushirikiaha wenzao hususani sehemu zenye mashamba makubwa na vitega uchumi vya biashara.....
Utashi wa kutenda kwa baadhi ya walimu haupo tena.Yaani mwalimu yupo kijijini lakini hana kuku,bustani au shamba ili iwekichocheo kwa yeye kutoa somo lile mashuleni.....
Hata hivyo zipo baadhi ya shule hazina kabisa EK au kipo ila kipo jina hivyo kupelekea kutokuonekana umuhimu wake.....
MWISHO
Nizipongeze shule zote zenye EK na kuzitendea haki na serikali ione hili ili kutilia mkazo suala la EK mashuleni......
Nakama kweli tunaitaji tanzania ya viwanda na kuongeza ajira kwa vijana basi serikali haina budi kutilia mkazo ELIMU YA KUJITEGEMEA.......