Ijue mizimu

Mr. Sound

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
2,217
Reaction score
4,800
Salam,

Mizim ni ma-spy wa kiroho, wanaowakilisha falme za kiroho kutucolonize.

Mizimu hujifungamanisha na koo zetu kwa kujifanya ndugu zetu waliokufa.

KAZI ZA MIZIMU
1. Kudumisha utumwa kupitia matambiko.

2. kututumikisha kupitia uchawi na uganga.

3. kukusanya taarifa zetu ajili ya kurahisha kutucolonize

4. kutufanya watumwa wa mila na desturi za kishetani

Nawatakia siku njema.
 
Ni kweli mizimu lengo lake ni kutawala wanadamu kwa ajili ya kufanikisha malengo ya ulimwengu wa giza. Mizimu hutumikisha watu kupitia sheria wanazotunga kwa wanadama na kwa njia ya kuwajengea wanadamu imani flani flani na zinazojenga hofu na hatia pale mtu anapovunja sheria zao. Mizimu huathiri maisha ya mtu pale anapokiuka sheria/masharti yao. Mizimu huweka sheria zao kupitia mfumo wa imani na utamaduni wa wanadamu. Ukiwa mtu wa kabila A utahukumiwa kwa mfumo wa sheria na imani za kabila A.

Unajiondoaje kwenye utumwa wa mizimu?
  • Ni kwa kuachana na imani, mila na tamaduni potofu.
  • Kataa kumilikiwa na kutawaliwa na imani na makatazo (taboo) ambazo hazitokani na Universal God (Mungu Mwenyezi) ambaye sheria zake ni za asili na kulenga kumweka binadamu huru na pia kuto kumhukumu binadamu kwa mambo ambayo sio kweli.
  • Shika sheria ya WEMA na UPENDO kwa wote na katika yote.
  • Amini na jua kuwa wewe ni mtawala na sio mtumwa katika dunia hii.


Asante ndugu yangu,naweza vipi kuiepuka?
 
Mkuu fazili umejibu vyema sana na kumpa mwongozo mzuri ambao akiufuata atafanikiwa kutoka ktk utumwa wa mizimu.
 
Katika ulimwengu wa Roho (modern spiritualism) ?” Waebrania 1:4.TK 337.1
Dhana kuwa Roho haifi ndo umizimu
Imani kwamba roho za wafu zinarudi kuwahudumia waliohai imefungua mlango kwa ajili ya imani ya kisasa ya mizimu.
Ikiwa wafu wanapata fursa ya kuwa na maarifa yanayozidi yale waliyokuwa nayo wakiwa hai, kwa nini wasirudi duniani ili wawafundishe walio hai? Ikiwa roho za wafu huvinjari juu ya rafiki zao duniani, kwa nini zisiwasiliane nao?
Ni kwa namna gani wale wanaoamini kuwa mwanadamu anajitambua baada ya kifo wanaikataa “nuru ya Mungu” iliyoletwa na roho wenye utukufu? Hii ni njia inayotiliwa maanani kuwa ni takatifu ambayo kwayo Shetani anafanya kazi. Malaika walioanguka wanaonekana kama wajumbe kutoka katika ulimwengu wa roho.TK 337.2

Mkuu wa uovu anao uwezo wa kuleta mbele ya wanadamu mwonekano wa rafiki zao waliokufa. Sura ya bandia itaonekana ni kamilifu, imetengenezwa kwa ubainifu wa ajabu. Wengi wanafarijika kwa uhakika kwamba wapendwa wao waliokufa wana fursa ya kuwa mbinguni. Pasipo hisia za hatari wanasikiliza, “roho zidanganyazo” lTimotheo 4:1TK 337.3

Wale waliokufa pasipo matayarisho wanadai kuwa wana furaha na wanashika nyadhifa za juu mbinguni. Hawa wageni wakujifanya kutoka kwenye ulimwengu wa roho wakati mwingine wanatoa maonyo ambayo yanathibitika kuwa ni sahihi. Kisha, kwa sababu wameaminika, wanaleta mafundisho yanayoshusha hadhi ya Maandiko. Ukweli kwamba wanatoa baadhi ya kauli za kweli na pengine kubashiri matukio ya siku za usoni unawafanya kuaminika, na mafundisho yao potovu kukubalika. Sheria ya Mungu imewekwa kando, Roho wa neema amedhihakiwa. Hizo roho zinaukataa Uungu Wakristo na kumweka Mwumbaji daraja moja na wao. Wakati ni ukweli kwamba matokeo ya hila yamekuwa na ushawishi kana kwamba ni udhihirisho wa kweli, kumekuwa na maonesho wazi ya nguvu za miujiza, ambazo ni kazi za moja kwa moja za Shetani. Wengi wanaamini kuwa imani ya mizimu ni ulaghai tu wa wanadamu. Watakapokutana uso kwa uso na udhihirisho ambao watauona kama miujiza, watadanganyika na kuukubali kuwa ni uwezo mkuu ya Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…