Kuwa mpole tu dada Furaha, mapenzi hayana formula inayofanana unaweza kusema miezi 7 ni mingi kumbe kwenye mazingira mengine ni michache sana. Umeeleza kwa urefu ila sijaelewa kama kwa sasa mnaishi pamoja au kila mtu kwake? Mnaishi pamoja na huyo dada ya mume mtarajiwa kwa sasa au mume anaishi na dada na wewe upo kwako? Anyway, take your time dada yangu, kama ni wako atakuwa wako tu la muhimu wewe play your part, kama kwa kumuheshimu, huo usafi anaotaka, mapenzi ya kweli na kadhalika. Kama unampenda na unadhani anafaa kuwa mume stahiki huna haja ya ku-rush, tekeleza wajibu wako.