Kuna Mwanamke mtaani ni anakaa jirani na nyumbani kwetu siku za mwanzo nilikuwa nikikutana naye dukani napokwenda kununua ...
Nikiacha kukuuliza umri, nikuulize unachomiliki chenye kuonekana katika jamii, mf: duka ama biashara nyingine yoyote ile, una kazi yenye kuheshimika?
Haujawahi mfanyia vitimbi ama dhulma yoyote ndugu ama rafiki yake?
Upo smart kwa turn out yako, yaani upo soap soap unajipenda?
Moja wapo ya sifa kwa maswali niliyokuuliza, yaweza kukupa thamani ya mwanamke kujilengesha, kwa heri ama kwa shari.
Si kila jino unalokenuliwa usidhani ni la upendo, maana hata hasidi aweza kukufanyia hivyo ili kuficha hila ovu moyoni mwake.
Nashauri kama umempenda, mtongoze dhahiri ili upate msimamo wake uweze kupima mustakabali halisi.
Kama atakuwa alikutega kimaslahi hapo ndipo utakapomgundua baada tu ya makubaliano, maana "demand" zitaanza kumwagika.
Sitaki kusikia unajihusisha na mke wa mtu.