HUU NI UNYANYASAJI. Please DONT TRY THIS

Mcheza Karate

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2011
Posts
690
Reaction score
354
Habari na poleni kwa kazi!!

Kuna jambo naona leo niliweke wazi, tushauriane na kuwekana sawa.

Kuna hili suala la wahudumu wa hoteli, nimekuwa nikifuatilia na kujiuliza maswali lukuki.

Ni kweli wamiliki wa hoteli wanahitaji faida na wanafanya biashara. Lakini kwa nini wafanywe vituko na kama chambo?

Wahudumu na mahotelia wengi ni wa kike tena-:
-wanamakalio makubwa,
-wanajikwatua
-wanavalishwa vibaya.

Hivi wewe dada yako akiwa na makalio makubwa halafu akavalishwa kisketi kama cha mtoto utafurahi?


kwangu kuona wahudumu hawa ambao wengi wana miili mikubwa kuvalishwa 'nguo za watoto' ni kama kituko na kudhalilisha utu wa mwanamke.

Kwani wateja hawaji hadi mdhalilishe wenzenu kwa vile tu mna vijisenti?

Acheni udhalilishaji. Na mnaotaka kufanya msijaribu. Mapaja na makalio ya dada zetu sio sehemu ya utalii wa ngono.

Alamsiki!
 
Kuwa na makalio makubwa ni kudhalilishwa?

Kujikwatua ni kudhalilishwa? Anakwatuliwa au anajikwatua mwenyewe?

Na kuhusu kuvalishwa vibaya sijui nisemeje, hívyo vimini ni kiasi gani? Na je wanalazimishwa?

Sema tu, mazingira yao ya kazi yako kkwenye mood mbaya za wateja, bbaada ya kazi anataka ajipumuzishe.
 
vaeni leggings. hata ukiwa na sketi fupi, hautaonesha maungo hadharani
 
Sisitiza dada zako wasome kwa bidii ili wasivalishwe visketi. mbona manesi nao sketi zao zinakuwa juu ya magoti hatusemi
 
Wateja mngekwa mnagome hizo sehemu unazani wamiliki wasingechukua hatua? Kuna chobingo za waarabu hapa hapa dsm wahudumu wamvaa midera na vilemba. Wamejistiri kupita maelezo coz wateja wao wanaendekeza arabic culture.

Sasa sie wateja tunaoendekeza culture ya vigodoro tusilalamike.
 
kwahyo unataka ulete changes? bas wahudumu wote wa mahotel wawe wanaume...
 
Hivyo vimini we umeviona huko mahotelini tu??????????? Ukishajijibu ndo ujiulize kama kweli watakuwa wamevalishwa? Mbona mahoteli kibao tu hapa mjini tunaonaga mpaka maustadhat na vishungi vyao wanafanya kazi?? Washawahi kukwambia wanalazimishwa??

Si ajabu wenyewe wanaona zile bado ni ndefu.........
 


Well said.....kumbe unakunywa soda gani vileee???
 
Mtuu kuvaa sketi fupi ni uhuni ujue anavutia biashara
 
wala hawalazimishwi kushona nguo fupi wahudumu wenyewe wanataka kuvaa hivyo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…