Huu ni ugonjwa gani?

Pawa chilonda

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2017
Posts
375
Reaction score
438
Nawasalimu wakuu Kuna ndugu yangu ameumwa Amoeba, Malaria na UTI

Sasa anatumia dozi lakini dozi zinaisha kesho Ila Kama siku tano nyuma anawashwa ngozi akijikuna vinatoka vipele vidogo vidogo katika mwili wake kachomwa sindano moja ya mzio lakini wapi amepewa na vidonge vya mzio wapi ndo vinazidi kutoka

 

Poleni, ningependa kuona picha ya sehemu flat kama mgongo au tumbo. Lakini, naweza kusema ni viral exanthema, huandamana na homa kali, vipele vyekundu vinawasha sana. Huweza kutokeza alama zake kwenye viganja na nyayo pia huweza sababisha maeneo hayo kuonekana yamejaa kidogo.
 
Picha ya mgongo mgonjwa kajipiga mwenyewe maana nipo mbali nae kidogo Ila anaehitaji msaada maana vinamuasha sana
 
Huu ni ubavu
 
Anatumia dawa gani katika hiyo dozi yake hyo mtu ?

Je kabla ya kutumia hizo dawa alikuwa anapata hii shida ?
Sasa anatumia dozi lakini dozi zinaisha kesho
Kesho ni siku ya ngapi tokea aanze kutumia dozi ?
 
Huwo ni ugonjwa wa zina ni atari sana nenda hospitali mapema
 
Hiyo ni aleji ya hizo dawa alizotumia,

Arudi hospital akaongezewa dozi ya sindano ya mzio.

Lakini pia zile dawa alizoandikiwa mwanzo za kutibu amoeba sijui uti asizitumie tena badala yake aende wakambadilishie wampe zingine.

Anywe maji kwa wingi,Asikate kwenye joto, Asivikune.

Hali hiyo huwa inaweza kumchukua hata mwezi hadi kuja kukaa sawa.

Kwa hiyo aendeelee na sindano za mzio.Abadili hospital aende hospital kubwa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…