Huko Bujumbura

Warundi ni watu wanaojitahidi sana kutumia lugha ya Kiswahili
 
Hao ndugu zetu hawakipendi kabisa sijui kwa nini!

Nilishawahi kuwauliza wakanambia kuwa kwao kiswahili hakipendwi kwasababu wanaona ni lugha ya kikatili, ni lugha ya vita. Hii ilitokana na ukweli kwamba wakati wa vita Amini wanajeshi walikuwa wakikitumia sana wakati wakiwakamata, kuwabaka na kuwatesa raia.
 
Sidhani kama ni sahihi kuwashangaa Warundi kushindwa kwao Kiswahili ilhali hata hapa jamvini wapo watanzania wanaongea stupidly

MSHAHALA
MUNAKWENDA
TUWACHENI TUPUMUWE
KUWADHARIRISHA
KUMTEKELEZA MTOTO n.k
 
You have a point there mpendwa...nadhani nyongeza pia huenda ni chuki yao dhidi ya Taifa la Tanzania in connection with Kagera War
 
Sidhani kama ni sahihi kuwashangaa Warundi kushindwa kwao Kiswahili ilhali hata hapa jamvini wapo watanzania wanaongea stupidly

MSHAHALA
MUNAKWENDA
TUWACHENI TUPUMUWE
KUWADHARIRISHA
KUMTEKELEZA MTOTO n.k

afadhali umeliona hili!!!
 
Hao ni wanafiki na waongo wakubwa. mbona Waingereza waliwatawala wakawabaka, kuwatesa na kuwafanya watumwa wa Daraja la tatu, zaidi hata ya Amini ktk nchi yao wenyewe lkn bado wanawapenda na kiingereza wanakipenda?
 
Hilo ndio hasa suala la kujiuliza!
 
Hao ni wanafiki na waongo wakubwa. mbona Waingereza waliwatawala wakawabaka, kuwatesa na kuwafanya watumwa wa Daraja la tatu, zaidi hata ya Amini ktk nchi yao wenyewe lkn bado wanawapenda na kiingereza wanakipenda?

Sio unafiki, kama unavyosema. Waingereza hawakufanya ukatili kiasi hiki kama ilivyo Kenya, Zimbabwe etc. Tayari waliwakuta watu wanajitawala wenyewe. Baada ya uhuru wao walikazana na kujifunza Kiingereza sio kama hapa kwetu Tanzania. Kiswahili kwao kilikua kinatumika na wanajeshi na polisi (hadi leo) na kama unajua historia ya Uganda ya miaka 70 and 80 wanajeshi walikua wakatili ndo maana watu wa miaka hiyo walichukia kiswahili. Kumbuka lugha ni mawasiliano, tayari wengi wanaweza kuongea kingereza kwahio kujifunza kiswahili kidogo ni added advantage.
Kumbuka pia lugha inategemea na jamii. Kiswahili ya Zanzibar na cha Mbeya au Bukoba ni tofauti. Kiingereza cha India au Australia na Merikani ni tofauti.
 
Mimi sina tatizo na wao kujifunza au kutokujifunza Kiswahili huo ni uamuzi wao na wala hawana haja ya kueleza kwa nini, kwa maana inaeleweka Kiswahili hakiwahusu, ila shida inakuja pale mtu anapoanza kuleta sababu zisizo na msingi, hivi unafikiri Bw.Iddi Amini asingezaliwa Waganda leo hii wangekipenda Kiswahili?

Kuhusu Waingereza, unavyosema SIO kweli, Afrika hakuna Ukoloni ambao haukuwa na Ukatili tena kupindukia, Waingereza wamechinja sana Uganda wala usitake kuwatetea, unajua ni Waganda wangapi wamekufa kwenye ujenzi wa Reli Mombasa- Uganda? Unajua ni wangapi walikuwa wanapigwa tu risasi kwa kuwa walikuwa wagonjwa na hawakuweza kufanya kazi? na mpaka leo tunavyoongea Waingereza bado wanachinja, kubaka, kuiba huko Uganda sana tu, hivyo sababu yao haina msingi wowote, na kama nilivyosema hapo juu hawapaswi hata kutoa sababu kwa nini hawakipendi Kiswahili, ni kama vile mimi pia sipendi Lugha yao ya Kiganda sasa sihitaji kutoa sababu kwa nini siipendi, kwa maana hainihusu na siihitaji kwa lolote sasa ni ya nini kwangu!
 
Hao ndugu zetu hawakipendi kabisa sijui kwa nini!

Huko kwa Kaguta nimeshuhudia kwa miaka ya hivi karibuni Kiswahili kimeanza kutumika sana katika mawasiliano kwa watu wa kawaida mitaani, tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma. Hata hivyo kwa wale "walioenda shule" ni nadra kumpata mtu anayeweza kuongea hii lugha.
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…