Naomba kuulizia uwezo wa hii gari katika kusafiri masafa ya mbali maana nimevutiwa na ulaji wa mafuta(1.6L ingine size) pia bei yake si mbaya (mfano gari ya mwaka 2000 inauzwa kwa FOB -2000 USD.) Zaidi ina umbo/size kubwa ukilinganisha na magari mengine yenye ingine size hiyo(1.6L).
Zaidi naomba nijuzwe upatikanaji wa spare za hii gari na bei ya hizo spare zake.....
Mkuu ulizia kingine na siyo swala la masafa marefu, enzi hizi magari yote yanakwenda masafa marefu vinginevyo hilo gari liwe bovu kwenye cooling system. Bajaj yenyewe inasafiri masafa marefu, itakuwa gari!
Mtoa mada umefanya vema, ngoja niwe around nipate kujua zaidi kuhusu hii model ya CRV hapa Tz kuitunza kwake inakuaje. Kikubwa ningependa kujua garage zake za uhakika tukichilia zile kubwa kubwa.
Pia sio mbaya waliowahi kumiliki wakatueleza kuhusu matatizo yanayowakumba mara kwa mara.