Una akili sana!! Kifo kipo tu kama ukumbusho kifo kipo mda wowote ule ila Kuna stage inafika nasi tunakuwa tunangojea kufa yaani miaka mingi ukifika kama utajaaliwa kuanzia 100 utakuwa umechoka ....so lipi la kujifunza? Ni kwamba hapa duniani ni sehemu tu tunaishi japokuwa tuna utofauti wa elimu, dini, utaifa, kipato ,akili na maendeleo but final njia yetu ni moja kwamba despite ya vitu vyote ivyo sisi sote tuko sawa na njia ni moja ...
Nini tufanye haijalishi itakuwaje ila lazima tuishi kwa upendo, tupunguze majigambo, kiburi ,ujuaji , dharau na kujifanya tuko juu...unaweza kuvimba hapa uko safi kesho tu umeparalyze huwezi hata kunyanya kidole cha mkono ni nusu ya maiti kabisa hapo ujanja kwisha.....Tutafute pesa na maishi bila kumkwaza mtu tutumie njia za halali tuache dhuluma ,utapeli , uwizi yote yanaweza kupelekea mwisho mbaya..
La mwisho hatujui Lin tunakufa ila tuombe mwisho mwema kwa uwezo MUNGU.